Thursday, March 5, 2009

Makumbusho ya Taifa - Dar es Salaam.
Nchi yetu ina historia kubwa sana ambayo inapashwa kuhifadhiwa kikamilifu ili vizazi vijavyo viweze kuelewa tumetokea wapi kwa maana ya kwamba ni rahisi sana kwa kumbukumbu hizi kupotea na kusahaulika kama hazikupewa uzito unaostahili.
Pengine naweza nisiwe na habari sahihi kuhusu Makumbusho haya ya Taifa, lakini sidhani ya kwamba jengo lililopo kwa sasa linatosheleza. Kama nitakuwa sahihi, basi nadhani iko haja ya serikali kufikiria ujenzi wa JUMBA la uhakika la MAKUMBUSHO YA TAIFA.

No comments:

Post a Comment