Wednesday, April 15, 2009

Raisi Kikwete akiwa katika picha ya pamoja kutoka kushoto - Nahodha Vuai(Waziri Kiongozi-Zanzibari), Shein(Makamu wa Raisi) na Karume(Raisi wa Zanzibari).
Uchaguzi Mkuu nchini mwetu huko njiani na bado mpaka wa leo hatujaweza kulipatia ufumbuzi lile suala linalojulikana kama "Matatizo ya Muungano". Ukitizama kwa undani sana utaona ya kuwa hatutaweza kulitatua tatizo la muungano bila ya kwanza kutafuta ufumbuzi wa mvutano kati ya visiwa vya Pemba na Unguja. La kwanza linalotakiwa kufanyika ni kufikiria nani aingie baada ya Karume kumaliza. Hili linatakiwa lifanyike kwa busara sana kama kweli tuna nia ya kuuendeleza huu muungano. Kisiwa kipi atatoka na ni nani atafuata baada ya Karume ni muhimu sana kuzingatiwa. Kuna uwezekano sana wa kuwa na majina mengi watakaotaka kuwania Uraisi Zanzibari, ikiwa ni pamoja na Waziri Kiongozi wa sasa, pamoja na kina Bilal, Sharif Hamad na wengineo lakini Shein anaweza kuwa ndio chaguo zuri zaidi. Usalama na Uimara wa Tanzania uko ndani ya Muungano na ndio maana tunauhitaji uendelee kuwepo.

No comments:

Post a Comment