Wednesday, September 30, 2009

Kule kwetu Tanga hivi vimgahawa viko kibao na uwa na chakula kizuri sana. Hapa utapata wali wa nazi na mandondo(maaragwe) na samaki wa kukaanga kwa bei poa kabisa, lakini tatizo ni kuhusu suala nzima la kiafya. Na sidhani kwamba hawa kina mama ntilie wanakuwa na leseni na hivyo hata suala la kuwakagua linakuwa halipo kabisa.