Unaposafiri kwenye mabarabara yetu mengi kuelekea mikoani ni lazima utakutana na watu wanaofanya biashara hii ya mkaa kando kanda mwa barabara. Pamoja ya kwamba mkaa ni muhimu katika matumizi ya kila siku huko majumbani mwetu, lakini vile vile biashara hii inaatharisha kuwepo kwa hali mbaya ya mazingira(mazingara?). Ukweli ni kwamba hao wanaofanya biashara hii wanakata miti kwenye misitu na mapori yetu, pengine ingekuwa vizuri kama watu hao wangefikiria kuwa na mashamba ya miti badala ya kuvamia kiholela misitu na mapori ya asili.
No comments:
Post a Comment