Tuesday, October 6, 2009

JIPATIE TOVUTI BURE KABISA

Pole na kazi ya kuelimisha na kuburudisha jamii yetu. Tumekuja na huduma mpya ya BURE kwa watanzania tu tunaomba uwafahamishe.

Kuzingatia umuhimu wa kuwa na tovuti, na ya kwamba ni gharama sana hapa TZ kupata tovuti, na tena watu wanafanya biashara rasmi kwa barua pepe za bure kama yahuu na giimeili, hii yote inaonesha ukosefu au gharama kubwa ya kupata tovuti. Sisi tumedhamiria kubadili uelekeo mzima wa upepo, na tumepata wasamaria wema na sasa rasmi tumefanikiwa kuleta ufumbuzi na neema kwa waTZ kwa suala la tovuti na anuani rasmi za barua pepe.

Na sasa kwa awamu ya kwanza kwa kuanzia tu, WATU 100 WATATENGENEZE WATOVUTI BURE. Watu 100 kwa maana ya mtu binafsi, kampuni, biashara, shirika, asasi zisizochukua faida (NGO), kikundi, duka, mjasiriamali, saluni, shule ama Saccos n.k.

BASI KILA ALIYEDHAMIRIA KUWA NA WEBSITE/TOVUTI ajiunge na utaratibu huu wetu atengenezewe TOVUTI MOJA BURE KABISA. TOVUTI HII YA BURE itamfanya mhusika aweze kupata anuani rasmi za baruapepe, yaani kama yeye ni Mwanahawa wa Vinyago Suppliers anatengenezewa anuani zake za barua pepe mfano mwanahawa@vinyagosuppliers.co.tz n.k kadiri ya atakavyo, nyingi apendavyo. Ataimiliki tovuti na kuiendesha yeye.

Kumbuka kwa awamu hii ya kwanza TUNATOA BURE TOVUTI 100 TU kisha awamu pili tunakuwa na kurasa mia moja zinazoelezea watu/kampuni/vikundi mbalimbali na shughuli zao hapa Tanzania, hii ni hatua kubwa sana na inaongeza maingizo ya utafutaji wa vitu toka Tanzania katika search engines na tunasogea mbele taratibu.

Hakuna vigezo vya kupata huduma hii ya bure, na tutahudumia kwa mujibu wa FIFO (first in first serve/out) wa kwanza kuja, wa kwanza kutoka/kuhudumiwa.

Maelezo na ufafanuzi zaidi tafadhali tembelea http://www.tovutiyangu.com ujisomee huduma hii kwa undani. Zipo pia huduma na bidhaa mbalimbali kwa walio na tovuti tayari.
Ahsante sana.

Admin,

No comments:

Post a Comment