Monday, October 5, 2009

Wakati Chama Cha Mapinduzi(CCM) kinazaliwa pale Arusha mwaka 1977 baada ya muungano wa Tanu na Afro Shirazi, wengi tulikuwa na matumaini kwamba nchi yetu ilikuwa ina mwelekeo fulani, kwa sababu kilizaliwa chama cha wakulima na wafanyakazi(na ndiyo sababu ya kuwa na jembe na nyundo). Leo sio hivyo tena! Ni chama cha MATAJIRI... na kimewasahau kabisa wakulima na wafanyakazi. Pengine inawabidi hawa viongozi wetu wa chama wakarudie kale kakitabu ka "AZIMIO LA ARUSHA" ili waone nini wanakosea. Kakitabu hako kana misingi mizuri sana inayopinga RUSHWA NA UFISADI pamoja na miongozo mingine mingi mizuri. Kama Wana-CCM na Watanzania tutaendelea kuyapuuza yale aliyoyasema Mwalimu pale Kilimanjaro Hoteli kabda ya uchaguzi uliomuingiza Mkapa madarakani, basi tujue ya kwamba tunaelekea kubaya.