Friday, March 26, 2010

Hii sehemu ya kugongewa idhini ya kuingia nchini(Visa) katika Kiwanja cha ndege cha Kimataifa(?) cha Mwalimu Nyerere ina utata kidogo. Kwanza, hakuna kipoza hewa na katika majira kama haya kunakuwa na joto la ajabu. Pili, ni padogo mno kuweza kuhimili abiria wengi na Tatu, bado baadhi ya hawa askari wa Uhamiaji na wa ushuru wana usumbufu usio wa lazima. Labda kwa sisi wenyeji tumeshayazoea hayo, lakini kwa wageni ambao tunataka sana waje nchini mwetu mtazamo wao ni tofauti kabisa. Kama bado tunataka waendelee kuja kwa wingi zaidi, basi tunahitaji mabadiliko. Tukumbuke kuwa wageni hawa wanapoondoka na kuizungumza vizuri nchi yetu kwa jamaa na warafiki zao ndivyo watakavyokuja kwa wingi zaidi.

No comments:

Post a Comment