Friday, July 30, 2010

Maswali ya Jino kwa Jino !
Radio Free Africa ya mwanza ! na Ras Makunja kamanda wa Ngoma Africa Band!

Radio Free Africa ya Mwanza ! Yawaletea mahojiano maalumu

Na Ras makunja kamanda wa Ngoma Africa Band siku ya

Jumamosi 31-07-2010 saa 4 hasubui

Habari za uhakika zinaeleza kuwa kituo cha Redio Free Africa kinachorusha matangazo yake mjini Mwanza, kitafanya mahojiano na Mwanamziki mashuhuri Ebrahim Makunja alimaarufu kama Ras Makunja kamanda wa ffu! wa bendi maarufu barani ulaya "The Ngoma Africa Band" yenye makao yake Ujerumani.

Mahojiano hayo yataanza saa 4 hasubui siku ya jumamosi 31-07-2010 katika kipindi maalumu ambacho mtangazaji wa redio hiyo Prince Baina Kamukulu ataongoza timu ya kumlima maswali Ras Makunja,mwanamziki ambaye ametajwa mara nyingi na vyombo vya habari vya ndani na nje nchi kuwa ni mtunzi mwenye hoja nzito kwa jamii,mara nyingine nyimbo zake utoa cheche za moto na kuwafanya walengwa wanao perekewa ujumbe wasipate usingizi!

Radio hiyo itamrusha hewani Live Ras Makunja, ambae ndie mpishi wa nyimbo nyingi ikiwemo CD yao mpya "Jakaya Kikwete 2010" CD ambayo imeshaingia nchini na inaweza kutingisha anga wakati wowote!

Wasilizaji zaidi ya milioni 200 wa afrika mashariki na kati wanatarajiwa kusikiliza mahojiano hayo ya Radio Free Africa na Ras Makunja,mahojiano ambayo yanatabiliwa kuwa yatakuwa ya "Jino kwa Jino" au "Jicho kwa Jicho" wewe msikilizaji usikose kuyanasa mahojiano hayo kambambe.

1 comment:

  1. Kamanda Ras makunja aka bwana kichwa ngumu,nimatumaini yetu kuwa katika hoja na mahojiano yako,utazungumizia maswala ya maana yatakayo wafungua macho watanzania wengi.
    tunaamini wewe ni moja wa wanamziki wachache sana
    wenye hoja nzito na mziki mkubwa

    ReplyDelete