Ndugu Watanzania na ndugu mlio karibu na Watanzania,
Mimi ninaitwa Dr Mariam Abu, mkazi wa Yonkers, NY. Kwa Tanzania mimi ni mkazi wa Mwananyamala, Dar-Es-Salaam na mwenyeji wa Tabora.
Napenda kuwakumbusha na kuwahamasisha Watanzania wote muishio New York, New Jersey, Pennsylvania na Connecticut kuhudhuria mkutano wa jumuia yetu mpya ya Watanzania, the New York Tanzanian Community (NYTC), utakaofanyisha Jumamosi Aprili 30, 2011 kuanzia saa nane mchana, nyumbani kwa balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa.
Anwani ni 30 Overhill Rd, Mount Vernon, NY 10552.
Kama wengi wenu mjuavyo, kutakuwa na mkutano mkubwa wa kuchagua viongozi watakaotuwakilisha katika kufanikisha majukumu ya jumuia.
Kwa wale ambao hawajafika kwenye website, tafadhali nenda www.nytanzaniancommunity.org ili uweze kusoma na kuelewa nia, madhumuni na majukumu ya hii jumuia. Kwa kifupi tu, jumuia hii imeanzishwa na Watanzania na kusajiliwa rasmi Aprili, 2011. Nia kubwa ya jumuia hii ni kuwajumuisha, kuwaunganisha na kuwaendeleza Watanzania katika nyanja mbali mbali za maisha. Kumbuka, kulingana na katiba ilivyo sasa hivi, hutoruhusiwa kupiga kura, kama haujawa mwanachama wa jumuia. Tafadhali njoo na mchango wako wa uanachama wa dola 50 kwa miezi sita au dola 100 kwa mwaka mmoja. Hii ni jumuia isiyojali rangi, kabila, dini, jinsia au jina lako la mwisho. Hatutojali kama unatokea Dar-es-salaam, Nzega, Rufiji, Masasi, Kahama, Kibosho, Kibondo, Bukoba, Mafinga, Ifakara, Pangani, Pemba, or you completely don’t know where these places are - for one reason or another.
Nikiwa kama mmoja wa watanzania tuliopitishwa kugombea nafasi ya uraisi wa Jumuia, na mwanamke pekee kwa hivi sasa, napenda kuwaomba mfike katika siku na muda uliopangwa ili tuweze kuchagua viongozi watakaotuwakilisha. Finally, I think it will be quite rude if I end this message without asking for your votes :)
See you all on Saturday!
No comments:
Post a Comment