Wednesday, April 27, 2011




Jah Kimbuteh with Roots & Kulture Band


Muhasisi wa mwanzo wa mziki wa hisia kali " Reggae" Afrika ya Mashariki
Unapouzungumzia mziki wa Reggae au mziki wa hisia kali nchini Tanzania na Afrika Mashariki
jina la Jah Kimbuteh atuwezi kulikwepa, mwanamziki huyu mtanzania na bendi yake "Roots and
Kulture band,aliyoianzisha mwaka 1985.

Jah Kimbuteh ni mwanamziki wa mwanzo wa afrika mashariki kuanza kupiga mtindo wa Reggae
na kufanikiwa kupata umaarufu ndani na nje ya Tanzania,pamoja na kufanya maonyesho ya ndani ya
nchini Tanzania, Jah Kimbuteh na bendi yake "Roots and Kulture" walifanikiwa kufanya ziara za
kimziki katika nchi sita zilizokuwa mstari wa mbele katika ukumbozi wa Afrika,pia kufanikiwa
kufanya maonyesho katika nchi za ulaya kama vile Norway na Austria.

Mara nyingi mziki wake umekua ukiimbwa kwa lugha ya kiswahili na kingereza ,na ujumbe uliopo katika
nyimbo zake kwa miaka ya 1980s alikuwa anaimiza sana ukumbozi wa nchi za kusini mwa Afrika.
baada ya ukombozi huo Jah Kimbuteh aliendelea kutumia mziki wa Reggae na kuimba katika maswala ya
nayo husu jamii.

Jah Kimbuteh CD zake za mwisho ni "True Democrasy" na "I am The Lion" baada ya hapo amekuwa kimya
kwa mapumziko ya mda mfupi..lakini washabiki wake wamekua wakijiuliza lini? mwanamziki huyu muhasisi
Reggae wa Afrika Mashariki atapanda tena jukwaani na kuliendeleza libeneke..la Reggae?

swali hili atalijibu Jah Kimbuteh mwenyewe ambaye bado tegemeo kwa washabiki
labda tutafutieni 00255(0)752240938 au 0752240930

1 comment:

  1. Hmm is anyone else having problems with the pictures on this blog
    loading? I'm trying to find out if its a problem on my end or if it's the blog.
    Any responses would be greatly appreciated.

    Feel free to visit my page; crack password

    ReplyDelete