Sunday, May 1, 2011


HATIMAYE JUMUIYA YA WATANZANIA JIJINI NEW YORK YAANZISHWA NA KUFANYA UCHAGUZI WA VIONGOZI WAKE! 




 Pichani Mh. Balozi Sefue akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wapya wa Jumuiya. Kutoka kushoto ni Naibu Katibu(Shabani Mseba), Naibu Mwenyekiti(Dr. Miriam Abu), Mwenyekiti na mwanae(Hajji Khamis), Mh. Balozi, Katibu( Vincent Mughwai) na Mweka Hazina( Phillip Lwiza, CPA) na Bwana Anicetus Temba( Naibu Mweka Hazina) ambaye hayuko pichani.


Pichani Mh. Balozi akiwa na viongozi waliochaguliwa pamoja na viongozi wa muda ambao walifanikisha katika matayashiyo ya kuanzishwa kwa Jumuiya.


Mwenyekiti mpya, bwana Hajji Khamis akikabidhiwa rasmi katiba ya Jumuiya na aliyekuwa mwenyekiti wa muda Profesa Mtui.


Naibu Mwenyekiti Dr. Miriam Abu akila kiapo cha kujitolea kuiongoza Jumuiya  toka kwa mchungaji Mama Butiku.



Mara baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa, kina mama na baadhi ya kina baba walishangilia kwa mduara wa kimasomaso mwanangu usimuone...


 Kama ilivyo kawaida makulaji hayakukosekana!


 Vijana wa show ya "Growing Up African"  nao walikuwepo kuwakilisha.




 Na mimi pia nilikuwepo kushuhudia tukio hili nikiwa na Willy "Mutu"


 Mmoja wa wagombea akipozi wakati wa harakati za kuomba kura.


 Wadau kwa wingi wakiwa wanasubiri mambo yaanze...

Mmoja wa mgombea nafasi ya uongozi, Bwana Phillip Lwiza, CPA; akiwa anakula mapozi ya kuombea kura na baadhi ya wageni waalikwa.


 Wanajumuiya  wakiwa wanafuatilia kwa makini maelezo ya mmoja wa wagombea wakati wa kujieleza.


 Mgombea wa nafasi ya Ukatibu Bwana Shabani Mseba wakati wa kujieleza.

 Bwana Hajji Khamis akiwa katika hatua za mwisho za kampeni za kuomba kura.


Mwenyekiti wa muda Profesa Mtui akiwa anafafanua jambo,  huku Mh. Balozi, Katibu wa muda(Bw. Benson Mwakalinga) na Mchungaji Butiku wakifuatilia kwa makini.

 Wanajumuiya wakifuatilia uchaguzi kwa makini...



 Mheshimiwa Balozi Sefue wakati akitoa nasaha zake kabda ya shughuli za uchaguzi hazijaanza.



 Wanajumuiya wakiwa wanasubiri kwa hamu shughuli zianze.

No comments:

Post a Comment