Tuesday, August 16, 2011

Breaking !News !!!!!!!!!!!!!!
Leo !
WANAKIJIJI WA KIMBIJI YAVAMIWA NA WANAJESHI! NA KUVUNJIWA!
pamoja uharibifu wa mazao yao
 
Majira ya saa nne hasubui wanakijiji wa kimbiji walivamiwa na wanajeshi wa ulinzi (JW) na kuvunjiwa makazi yao pamoja na kuharibiwa mazao yao,
Malori manne yaliyojaa wanajeshi yalikivamia kijiji cha kimbiji nje kidogo ya Dar-es-salaam, na kuvunja vunja maeneo ya makazi ya wanakijiji hao ! wanajeshi hao walichukua hadi baadhi ya vifaa vilivyojengewa makazi ya wanakijiji hao na kupakia katika magari yao na kuondoka navyo !
 
Wanakijiji walipo jaribu kuuliza kulikoni waliambiwa kuwa nyinyi hamrusiwi kukaa katika eneo hili ! wanajeshi walidai kuwa eneo la kijiji hiko ni sehemu ya kupigia shabaha ya kijeshi !
 
Wanakijiji hao na uongozi wa serekali ya Kijiji hauna taarifa yoyote ya kisheria kutoka Serekalini ,Idara ya ardhi ,ofisi ya mkoa kuwa kijiji cha kimbiji kimepewa wanajeshi.
Mpaka tunaenda mitamboni kuandika habari hizi wanakijiji wa kimbiji hawajui wamlilie nani? kwa wanajeshi wanaopaswa kuwalinda wananchi wamekuwa mstari wa mbele katika kuwanyanyasa wananchi na kuwaaribia mali na makazi yao,kama vile nchi inatawaliwa  kijeshi!?
 
Uongozi wa serikali usipoingilia kati na kulaani vitendo hiki cha wanajeshi kuvamia makazi na kuaribu mali za wapiga kura,inawekana kabisa wananchi wakachoshwa na kero kama hizi na matokeo yake wakajiami ,au kutokea kama kilichotokea eneo la MADALE miezi michache mwaka huu.utafiti unaonyesha kuwa KIMBIJI haipo katika mpango wa kigamboni new town.
 
Kinacho jaribu kufanywa na wanajeshi ni kutaka kujichukulia ardhi kimabavu kwa kutumia nembo ya jeshi.kama ni hivyo basi serekali haraka sana ingilie kati kuwanusuru na kuwatetea raia wake ambao wameipigia kura serekali.

No comments:

Post a Comment