Wednesday, August 17, 2011

Uvamizi wa wanajeshi dhidi ya wanakijiji Kimbiji ! Polisi kigamboni wamekua BUBU!
hawajakubali kupokea malalamiko ya wanakijiji ! nani ? wa kumfunga simba kengele?
Kuanzia jana jumatano saa 4.00 hasubui wakazi kijiji cha Kimbiji,nje kidogo ya jiji la Dar, wamekuwa na mashaka ya maisha baada ya makazi na mazao yao kuharibiwa
vibaya na wanajeshi (JWTZ) ambao walivamia kijiji hiko na kuvunja vunja makazi ya raia..kinyume cha sheria.
 
Hata hivyo baadhi ya wanakijiji walipereka taarifa katika vya vituo vya polisi vya Kigamboni na mji mwema,havijakubali kupokea malalamiko ya wanachi walioharibiwa mali zao na kutishiwa usalama wao,hadi sasa inaonekana kuwa wanachi wa Kimbiji hawana wa kuwalinda wao na mali zao,kama inavyoeleza katiba ya nchi kuwa kila raia ana haki ya kupewa ulinzi wa maisha yake na mali zake!
 
Katika Sakata hili la wanajeshi (JWTZ) kuvamia makazi ya raia na kuharibu mali za raia bado lina utata wa nani ? kumfunga kengengele simba?

No comments:

Post a Comment