AIBU GANI HII BADO INAENDELEA KULIKUMBA TAIFA LETU!
Jeshi la Polisi nchini (PT) kupitia Inspekta Generali
wake Said Mwema(Pichani) imetangaza dau la Shilingi Milioni 5 kwa mtu yeyote
atakaefanikisha kupatikana kwa mtu aliyemjeruhi mtoto Adam Robert (14) ambaye ni
Albino huko Geita ambapo mtu asiyejulikana alimvamia mtoto huyo na kuanza
kumkata kata mikono na kisha kutoweka na vidole vya Albino huyo.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia mwishoni mwawiki
katika Kijiji cha Nyaruguguna, Kata na Tarafa ya Nyang’hwale ambapo mlemavu
huyo, Adam Robert (14), mwanafunzi wa darasa la nne, alivamiwa na kukatwa mkono
wa kulia na kisha kunyofolewa vidole vitatu vya mkono wa kushoto.
Ni
jambo la kusikitisha sana kuona vitendo hivi vinaendelea kutokea na mwisho wa
siku jeshi linataka kutumia fedha za walipa kodi kwa ajili ya kuwapata wahalifu
hao, mi nadhani hii njia sio sahihi, sidhani kama Jeshi la polisi wanashindwa
kuwapata hawa wanaowatuma wahalifu kwenda kuwadhuru maalbino hawa. Jambo la
msingi hapa sio kutangaza dau ni kuhakikisha wale wanaowatuma ndio wanakamatwa
na ninaamini jeshi la polisi likishirikiana na usalama wa Taifa inawezekana
kuwakamata hawa na kuwatokomeza kabisa, usalama wa Taifa wanafanya kazi gani
kama sio pia na kuangalia usalama wa Watanzania hawa!
Ni
aibu kubwa kwa Taifa letu vitendo hivi vinavyoendelea.
No comments:
Post a Comment