SAKATA LA MGOMO WA WANACHUO WA IMTU UNIVERSITY HATMA YAKE LINI?
Geti kuu la kuingia
Chuo kikuu cha Afya IMTU kilichopo Mbezi Beach.
Wanachuo hao hapa
wakiwa katika moja ya maandamano ya mgomo huo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr Shukuru
Kawambwa
Sakata hili
lilitolewa miezi michache iliyopita na vyombo mbali mbali vya habari kuhusu
mgomo huu wa wanachuo hawa.
Ni
jambo la kusikitisha sana kuona nchi ambayo ina upungufu mkubwa wa Madaktari,
kushindwa kuumaliza mgomo wa Madaktari Wanafunzi ambao sasa umekamilisha miezi
miwili, kundi hili la wanachuo limekuwa likikusanyika nje ya Makao Makuu ya
Wizara ya Elimu kwa vipindi tofauti bila hitimisho la mgomo huu.
Kwa
kutambua umuhimu wa wataalam hawa tunaziomba mamlaka zilizopewa dhamana ya
kusimamia na kuongoza ziumalize mzozo huu ambao madai yao ya msingi ni kulipa
Ada kwa Tshs na si US Dollar na pia kulipa ada kubwa tofauti na vyuo vingine vya
binafsi (private).
Sisi
kama wanafunzi ambao tunaathirika na mgomo huu Bado tuna imani na Serikali ya
Mh.Jakaya kikwete na watendaji wake wote, Katibu Mkuu Wizara ya elimu,Tanzania
Commision of Universties na Higher Education Student Loan Board tunawaomba
waumalize mzozo huu.
Pesa
nyingi zimetumika za walipa kodi kupitia loan board kuwakopesha wanafunzi hawa
Tunahitaji sasa wote kwa pamoja kulishughulikia hili tatizo ili tuweze kuendelea
na Masomo na mwisho tuende kujenga taifa letu changa lenye upungufu mkubwa wa
Madaktari.
No comments:
Post a Comment