HATARI ILIYO MBELE KWA WAMACHINGA WANAOONGEZEKA KWA KASI KATIKA MATAA YA UBUNGO SERIKALI MNAIONA?
Trafiki Polisi
akiongoza magari katika junction kubwa ya Ubungo, maarufu kama Ubungo Mataa.
Fuso ikiwa imeingia
katika moja ya mtaro mkubwa ulioko bara bara ya Ubungo karibu na Ubungo mataa.
Kwa kipindi kirefu
sasa eneo la Ubungo karibu na Mataa ya kuongozea magari yanayo ingia Jijini au
yale yanayotoka pande mbili, mengine yakitokea Mwenge na mengine yakitoke
Buguruni na kwenda sehemu mbali mbali za jiji limevamiwa na wafanya biashara
ndogo ndogo maarufu kama Wamachinga.
Nimejaribu
kulifuatilia kwa kipindi kirefu ili kuweza kujiridhisha kujua kama wamepewa
ruhusa na nani kufanya biashara katika eneo lisilo rasmi, nilijaribu kuongea na
wamachinga wachache; wa kwanza anaitwa Salum Ramadhan anauza taa za kichina
katika eneo hilo, yeye alidai hawajaruhusiwa na mtu kufanya biashara hapo ila ni
kutokana na ugumu wa maisha ndio umewapelekea kufanya biashara katika eneo hilo
na wa pili naye Ndg. Deogratius Shirima akasema maneno hayo hayo ambayo
hayapishani maana na huyu wa kwanza.
Sikuishia
hapo nikataka kujua je kuna mtu yeyote ambaye anakuja kukusanya japo ushuru
kutoka kwao? nao kwa pamoja wakasema kuna mtu huwa anakuja kukusanya ushuru
lakini wao hawana uhakika kama ni kutoka Serikali za mitaa au la! nikawauliza
swali jingine, huyu jamaa ambaye ameweka jenereta hapa na kuwapa huduma ya Umeme
mnamlipa Sh. ngapi? wakasema kila taa 1 ni Sh. 1000/- nikapenda nijue sasa swali
langu la msingi, wanajua HATARI
iliyo mbele yao kutokana na kufanya biashara kando kando ya bara bara kubwa kama
hii ambayo inapitisha magari mengi na hasa mengine yanakuwa yako kwenye mwendo
wa kasi! wakasema wanaifahamu ila hawana jinsi wataenda wapi na maisha yenyewe
ni magumu!
Kwa kweli nilitoka
bila kuwa na jibu sahihi nini hatma yao kama gafla gari likitoka kwenye bara
bara na kuwavama.
Tatizo hili naamini
serikali wanaliona ila wanalifumbia macho na pindi ajali itakapo tokea ndio
wanafumbua macho na kujua sehemu sio halali, ni vema serikali ikalichukulia
hatua mapema kabla halija tokea la kutokea. Tumekua tukiona sehemu mbali mbali
ajali zinatokea na kuua watu wengi ambao wapo kando kando ya bara bara kwa hiyo
ni vema Serikali ikachukua tahadhari mapema.
No comments:
Post a Comment