LEO NI SIKU ALIYOFARIKI BIBI TITI MOHAMED, MMOJA WA WANAWAKE WALIOKUWA WANAHARAKATI WA UKOMBOZI WA TAIFA LETU.
Bibi Titi Mohamed
enzi za uhai wake.
Hapa akiwa na Baba
wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Bibi Titi
Mohammed (1926 - 5 Novemba, 2000) alikuwa mmoja wa wanawake wa kwanza
kushika nafasi za ubunge na uwaziri nchini Tanzania. Pia alikuwa kati ya wanawake wa
kwanza kujiunga na harakati za kugombea uhuru wa Tanganyika.
Mwaka 1969 Bibi Titi Mohammed alikamatwa na
mwaka uliofuata alifikishwa mahakamani kwa kosa la kula njama ya kutaka kupindua
serikali. Katika kesi hiyo, Bibi Titi alikuwa ni mwanamke pekee katika
washtakiwa 7. Baada ya kesi hiyo kusikilizwa alipatikana na hatia na kuhukumiwa
kifungo cha maisha. Hata hivyo, mwaka 1972 alisamehewa na rais Julius Nyerere.
Juu ya kutolewa kwake, Mohammed aliongoza maisha
yake akiwa mpweke. Mume wake alimtelekeza wakati wa kesi, ushirika wake wa
kisiasa ukanyang'anywa, na marafiki zake wengi wakamlani.
Mnamo mwaka wa 1991, wakati Tanzania ikisherekea miaka 30 ya uhuru, Bibi
Titi ameonekana kwenye makaratasi ya chama tawala kama "Shujaa wa Kike Aliyepigania Uhuru".
Mnamo tar. 5 Novemba, 2000 Mohammed amekufa kwenye hospitali ya Net
Care Hospital mjini Johannesburg ambapo alikuwa akitibiwa.
Moja kati ya mabarabara makubwa ya mjini Dar es Salaam yamepewa
jina la Mohammed kwa heshima ya mafaniko makubwa aliyoyafanya wakati wa mbio za
kutafuta uhuru wa Mtanzania.
No comments:
Post a Comment