Saturday, March 24, 2012

Bonanza la Waandishi wa Habari Bongo lafana....

Wacheza Shoo wa Wanangwasuma FM Academia wakingwasumika katika Bonanza la waandishi wa Habari Tanzania linaloendelea mpaka hivi sasa likiwa limeandaliwa na TBL

Pamoja na Nchi yetu kuwa na matatizo ya hapa na pale kama Umeme kukatika na Madaktari kugoma lakini Watanzania bado wanaonekana kuwa na furaha. Hapa Waandishi wa Habari wa Bongo wakiserebuka katika bonanza lao lililoandaliwa na TBL katika Ufukwe wa Coco Beach

Amani na Vicheko mtindo mmoja ndani ya Bongo.....Waandishi wa Habari wa Tanzania wakifurahia ndani ya Bonanza lao linaloendelea sasa hivi katika fukwe za Coco Beach....Tamasha hilo limeandaliwa na TBL

Bibi Cheka akiyarudi mangoma na Mh Temba ndani ya Bonanza la waandishi wa Habari Tanzania katika fukwe za Coco Beach

Baada ya kujirusha sana na kuishiwa nguvu Bibi Cheka alianguka na kupoteza fahamu kwa furaha na hapa akipatiwa huduma ya kwanza ili arudi katika hali ya kawaida na kuendelea kujirusha katika bonanza la Waandishi wa Habari Bongo leo hii.

1 comment:

  1. Umetudanganya Media Day haijafanyika Coco Beach kama ulivyoandika, imefanyika Msasani Beach.

    ReplyDelete