Aliyekua msaidizi wa Katibu Mkuu wa UN Mh.Mama Rose Migiro akizungumza machache na Viongozi wa Jumuia ya Watanzania jijini New York katika Hafla maalum iliyoandaliwa na uongozi huu katika Kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kutumikia Umoja wa Mataifa. Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.
Mh, Asha-Rose Migiro anarudi nyumbani Tanzania baada ya kuitumikia UN kwa kipindi cha miaka 5. Mh Asha-Rose ni Mtanzania wa kwanza mwanamke kupata nafasi kubwa ya kufanya kazi katika Umoja wa Mataifa akiwa kama msaidizi wa Katibu Mkuu Ban Ki-Moon. Mh, Asha-Rose aliandaliwa hafla hiyo na uongozi wa Jumuia ya Watanzania hapa New York kama shukrani zao kwake ambaye alikuwa kama mlezi wa jumuia na alishirikiana na uongozi kwa hali na mali kila alivyo pata nafasi ya kufanya hivyo. Uongozi wa jumuia ya Watanzania New York unamtakia kila la kheri huko aendako na unategemea kuendelea kuwasiliana na kama mlezi.
MKATABA WA KELVIN YONDANI KWENDA YANGA NI BATILI - ADEN RAGE
Mwenyekiti wa Simba SC, Aden Ismail Rage akionyesha picha ya Yondani
akisaini mkataba na Yanga kwa wanahabari (hawapo pichani).
Simba
Sports Club imesikitishwa na kitendo cha Young Africans kuvunja
taratibu za usajili kwa kumrubuni mchezaji wake Kelvin Patric Yondani
kwa kuzungumza naye na baadae kwa ushahidi wa picha kuonekana
wakimuandikisha makaratasi ambayo baadae imeripotiwa na vyombo vya
Habari kwamba alikuwa akisaini mkataba wa kuichezea timu hiyo ya Young
Africans.
Chadema yatikisa CCM, CUF Lindi
Operesheni Okoa Kusini imevitikisa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama
Cha Wananchi (CUF) mkoani Lindi.
Abdallah Madebe, aliyekuwa Meneja wa
Kampeni za Mbunge wa Lindi Mjini, Salum Khalfan Barwan (CUF),
alijiondoa katika chama hicho na kujiunga Chadema.
Maombi ya Asubuhi
Mchungaji Peter Igogo anawakaribisha
ndugu wote katika huduma ya maombi ya asubuhi ambayo yanaanza rasmi
kesho june 6, 2012 asubuhi Kutakuwa na
awamu mbili za dakika 30. Awamu ya kwanza saa
11:30-12 asubuhi ( 5:30am- 6:00am) na awamu ya pili itaanza 12
asubuhi-12:30 asubuhi (6:00am-6:30am). Ni huduma kwaajili ya kuanza
vyema siku yako na uwepo na ulinzi wa Mungu.Muda huu ni Eastern Time kwa wale walioko Marekani.
Maombi ya ANZA SIKU YAKO NA BWANA maombi
haya yatafanyika kwa njia ya simu katika namba Tel:605 477 2100 password 640968 kwa
waishio Marekani kama upo nje ya Marekani anza na 01.
pia ninapatikana kwa namba Cell:301 377 3443. Njoo tuanze
siku na Bwana
Mungu na Akubariki sana
Mchungaji Peter Igogo
Cell: 301
377 3443
Tanzanian America Business Conference in Renaissance Hollywood Hotel
The Tanzania Investment Group of U.S.A, Inc. (TIGU) is a
collection of investors with a vision and mission to extend and develop
business relationships with diverse companies around the world. Started
from a modest beginning, a group of trustworthy business-minded men and
women realized that boundless potentials still exist in the world,
Tanzania in particular. TIGU seeks to develop business relationships
with potential investors around the globe.
Vision:
To become the most trusted business and management reform services and
products providers around the globe.
Mission:
TIGU is steadfast in ensuring a long-term commitment to dynamic
transformation with dedication to evolutionary growth of quality
products, services, functionality and improved returns at profitable
levels.
FASHION SHOW BY ASYA IDAROUS KHAMSIN
Contacts:
Tanzania Investment Group of U.S.A., Inc.
11336 Huston Street
North Hollywood, CA 91601
U.S.A.
ph: +1-951-333-9929
business@tiguinc.com
Register for
TIGU Inc. 2012 Tanzanian American
Business Conference
The Renaissance Hollywood Hotel
1755 North Highland Avenue
Hollywood, CA 90028
U. S. A.
JUZI Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison
Mwakyembe juzi alichukua uamuzi mgumu wa kutengua uteuzi wa Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Paul Chizi kutokana na kuteuliwa bila
kufuata taratibu zinazotakiwa na badala yake akamteua rubani wa siku
nyingi ndani ya shirika hilo, Kapteni Lusajo Lazaro kukaimu nafasi
hiyo.
Waziri Mwakyembe
alichukua uamuzi huo kutokana na taratibu za uteuzi kwa wafanyakazi wa
umma kutokufuatwa wakati wa kumteua Chizi.
Kabla ya kuteuliwa
kushika wadhifa huo na aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Omari Nundu
Chizi aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Community
Airline wakati taratibu zinasema, mtu anayetakiwa kukaimu nafasi hiyo
anatakiwa kutoka miongoni mwa wafanyakazi wa ndani ya shirika ua
taasisi.
Kiwanja kilichomng’oa Mkulo chaundiwa tume
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za
Mashirika ya Umma (POAC), imeunda tume ndogo kuchunguza uuzwaji wa
Kiwanja Namba 10 ambacho kilikuwa kinamilikiwa na Shirika la Usagishaji
la Taifa (NMC), kabla ya kuuzwa katika mazingira tata kwa Kampuni ya
Mohamed Enterprises (MeTL).
Kiwanja hicho ni miongoni mwa sababu
zilizomng’oa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo baada ya Ripoti ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuonyesha jinsi
alivyoshiriki kwa namna moja au nyingine katika uuzaji wa kiwanja hicho
huku akiivunja Bodi ya Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma (CHC) ili
kuficha tuhuma hizo
BAJETI: Upinzani kulia na kodi ya mishahara, vyakula
WATAKA MISAMAHA YA KODI IPUNGUZWE, KUIBANA
SERIKALI BUNGENI KUHUSU POSHO
KAMBI ya Upinzani Bungeni imetoa mwelekeo wa bajeti mbadala yenye vipaumbele 10, ikilenga kufuta misamaha ya kodi na kupunguza kodi ya mishahara na mazao ya chakula ili kukabiliana na ugumu wa maisha.Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa kambi hiyo itaishinikiza Serikali kupunguza misamaha ya mbalimbali ya kodi kutoka asilimia tatu hadi moja ya Pato la Taifa, huku kodi ya mishahara ya wafanyakazi (Paye), ikipunguzwa kutoka asilimia 14 hadi tisa.
Tayari Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa ametangaza mwelekeo wa Bajeti Kuu ya Serikali ambayo itatumia Sh15 trilioni, huku ikiwa na maeneo saba ya vipaumbele ikiwamo miundombinu ambayo imegawanyika katika makundi manne ya reli, umeme, usafirishaji na uchukuzi.
Wanaume wanaoongoza kwa kuvunja ndoa za watu-2
WIKI iliyopita utakumbuka nilianza kuzungumzia wanaume ambao
wamekuwa wakilalamikiwa huko mitaani kwa kuongoza kuvunja ndoa za watu.
Makala hii imetokana na uchunguzi wa muda mrefu ambao umeonesha kuwa,
kuna aina flani ya watu ambao wamekuwa na ushawishi wa hali ya juu kwa
wake za watu na hatimaye kutembea nao.
Nilianza kuwazungumzia madeveva wa teksi na bajaji, wauza magenge na maduka pamoja na walimu ambapo tumeona ni kwa jinsi gani wamekuwa wakiogopeka kutokana na tabia zao ambazo zimesababisha migongano katika ndoa nyingi
Nilianza kuwazungumzia madeveva wa teksi na bajaji, wauza magenge na maduka pamoja na walimu ambapo tumeona ni kwa jinsi gani wamekuwa wakiogopeka kutokana na tabia zao ambazo zimesababisha migongano katika ndoa nyingi
TANGAZO: Kikao cha mTanzania aliyeko hospitali
Kwanza tunapenda kuwashukuru wote walioshirikiana na familia kukutana na
hata kuwasiliana nasi kuhusu kikao kilichotangazwa kufanyika Jumatano
iliyopita (tarehe 30 Mei).
Kilifanyika kama ilivyopangwa na tunashukuru kwa wote waliohudhuria na
wale ambao waiwasiliana nasi kabla, wakati na baada ya kikao kueleza
kushindwa kuhudhuria.
Mpaka hivi sasa hali ya mgonjwa ilikuwa ikiendelea vema zaidi na hadi
kufika siku ya kikao, alikuwa ameondolewa hata dawa za maumivu makali
alizokuwa akitumia.
Baadhi ya maendeleo yaliyopatikana mpaka sasa ni pamoja na kushiriki
katika njia tofauti kuisaidia familia ya Bwn. Domitian Rutakyamirwa hasa
mke na watoto. Hii ni pamoja na mchango ambao ulikusanywa toka kwa watu
mbalimbali kusaidia gharama za matunzo ya mgonjwa na baadhi ya gharama
za familia yake.
Pia, kuna akaunti maalum iliyofunguliwa kwa ajili ya kusaidia gharama
kwa familia
Jina ni…. DOMITIAN CARE AND SUPPORT ACCOUNT.
Benki…. BANK OF AMERICA
Routing.. 052001633
Account.. 446026881993.
Bado Ndg Domi (kama anavyojulikana kwa wengi) anahitaji maombi pamoja
na dua ili Mwenyezi Mungu aweze kumuangazia. Amelazwa chumba namba 523
katika hospitali ya Chuo Kikuu cha George Washington iliyopo
900 23rd St., NW.
Washington, DC 20037.
Pamoja na maombi, Ijumaa ya wiki hii (June 8, 2012), familia ya Ndg Domi itakutana na ndugu, jamaa na marafiki kujadili masuala kadhaa kuhusu hali yake. Unakaribishwa kuhudhuria na kutoa mchango wako wa mawazo katika yale yatakayojadiliwa.
Kikao kitafanyika saa moja kamili jioni.
Anwani ni
10110 Greenbelt Rd,
Lanham,MD,20706
NYOTE MNAKARIBISHWA
Pamoja na maombi, Ijumaa ya wiki hii (June 8, 2012), familia ya Ndg Domi itakutana na ndugu, jamaa na marafiki kujadili masuala kadhaa kuhusu hali yake. Unakaribishwa kuhudhuria na kutoa mchango wako wa mawazo katika yale yatakayojadiliwa.
Kikao kitafanyika saa moja kamili jioni.
Anwani ni
10110 Greenbelt Rd,
Lanham,MD,20706
NYOTE MNAKARIBISHWA
Unaweza kuwasiliana na
Henry Kente: 240-938-2452
Bernadetha Kaiza: 240-704-5891
Mubelwa Bandio: 240-281-0574
TANZANIA REPRESENTED @ THE COMMONWEALTH LUNCHON WITH HER MAJESTY THE QUEEN ON WEDNESDAY, 6 JUNE 2012
H.M. The Queen receiving a present on
behalf Commonwealth heads of State and Government
Her Majesty the Queen poses with the
representatives of Heads of State & Governments from the
Commonwealth countries after receiving her present to commemorate her
Diamond Jubilee
H.E. Peter
Kallaghe Tanzania's High Commissioner to the UK poses in front of the
present that was presented to Her Majesty the Queen
Nice &
unique: A close up shot of the present that Her Majesty the Queen was
given by the representatives of the States and Governments of the
Commonwealth Countries
It reads:
"Presented
to Her Majesty Queen Elizabeth II by Heads of Government representing
the governments and people of the Commonwealth Nations to mark Her
Majesty's Diamond Jubilee as Head of the Commonwealth, symbol of our
free association.
Offered with
profound admiration and abiding appreciation for the manner in which
her Majesty has diligently and faithfully served the Commonwealth and
advanced it's values of democracy, development and respect for diversity
through six decades, as both head and the heart of the Commonwealth
Family, evoking the deep respect and affection of Commonwealth citizens
around the globe."
6th June
2012
Tanzania High Commissioner HE. Peter
Kallaghe with the former Commonwealth Secretary General, Sir Shridath
Ramphal
H.E. Peter
Kallaghe, with the President of
Nambia (centre), H.E. President Hifikepunye Pohamba
President of
Nambia H.E. Hifikepunye Pohamba poses for a photo with his spouse, Mrs Penehupifo Pohamba, second from
left, and spouse of Cameroon High Commissioner left, spouse of Tanzania
HC Joyce Kallaghe, Ivory coast, Nambia, Guinea and right Swaziland High
Commissioner
ZIARA YA NAPE NJOMBE, MKUTANO WAKE MAKAMBAKO WAFUNIKA
Katibu wa Halmashauri
Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia umati wa
watu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo, Juni,6, 2012
kwenye uwanja wa Polisi, mji wa Makambako, wilaya ya Njombe mkoa mpya wa
Njombe.
Nape akipiga ngoma
Katibu wa Halmashauri
Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia umati wa
watu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo, Juni,6, 2012
kwenye uwanja wa Polisi, mji wa Makambako, wilaya ya Njombe mkoa mpya wa
Njombe.
.Katibu wa Halmashauri
Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye , akizindua tawi la
CCM, Ubena Makambako, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama
mkoani Njombe.
Mzee Leonard Mwampamba akimkabidhi
mundu Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape
Nnauye, alipozungumza na wazee wa Ilembula, wilaya ya Wanging'ombe akiwa
katika ziara ya kikazi mkoani Njombe leo
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa
CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisakata muziki na kijana Kata ya
Ilembula, kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye Kata hiyo.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa
CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akizungumza na wazee wa Kata ya
Ilembula wilaya ya Wanging'ombea akiwa katika ziara ya kikazi mkoani
Njombe.
Nape akipuliza baragumu
la kienyeji wakati akishiriki ngoma wakati wa mapokezi yake Ilembula.
Vijana wakionyesha
umahiri wa kucheza sarakasi walipotumbuiza wakati wa mkutano wa CCM
kwenye uwanja wa Polisi Makambako.
BONDIA JAPHET KASEBA AZUNGUMZA NA MO BLOG KUHUSU 'FREEMASON'
MO
BLOG: Kaseba kuna
ukweli wowote kwamba kabla ya kucheza pambano ni vyema siku moja kabla
mtu unapaswa kufanya mapenzi.?.
KASEBA: Kwa kweli kwa kuwa mimi nilianzia kwenye mchezo wa
‘Martial Arts’ , hicho kitu kilikuwa kinapingwa sana na sidhani hata
katika michezo mingine kinakubalika. Sana sana ningewaasa watanzania
kujituma katika mazoezi na kuacha kudanganyana.
MO BLOG: Hebu izungumzie familia yako kwa sababu mengi yamesemwa
na hatupendi kuyarudia.
KASEBA: Nampenda sana mke wangu, nawapenda ndugu zangu,
pia nawapenda sana wazazi wangu na siku zote namshukuru mwenyezi mungu
na naamini hiyo ni moja wapo ya mafanikio yangu, kwa kuwa kila
ninachohangaikia nahaingikia kwa sababu ya familia yangu. Kusoma mahojiano yote Bofya hapa
SUPER D AENDEREA KUWAFUA MABONDIA WA KAMBI YA ILALA KWA AJILI YA MPAMBANO WA KUMI BORA JUNE 15
Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super
D' kulia akimwelekeza jinsi ya kutupa makonde bondia Said Mtitu wakati
wa mazoezi yanayoendelea katika Kambi ya Ilala Dar es salaam jana ya
kujitaharisha na mashindano ya kumi Bora yatakayofanyika june 15 katika
ukumbi wa Panandi Panandi Ilala Bungoni.
Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super
D' kushoto akimwelekeza jinsi ya kutupa makonde bondia Said Mtitu
wakati wa mazoezi yanayoendelea katika Kambi ya Ilala Dar es salaam
jana ya kujitaharisha na mashindano ya kumi Bora yatakayofanyika june
15 katika ukumbi wa Panandi Panandi Ilala Bungoni.Picha na www.superdboxingcoach. blogspot.com
Wednesday, June 6, 2012
BEAUTICIAN, DESIGNER, LINDA EXPRESS AVAA GWANDA
Linda Express (Mrs Mali Buzuidenhout) Jumatano June 6, 2012 mchana
alifika Hyattsville, nyumbani kwa Katibu wa CHADEMA, Liberatus
Mwang'ombe kuchukua kadi ya uanachama wa chama hicho ambacho kimefungua
tawi DMV siku ya Jumapili May 27, 2012 kwenye ukumbi wa Mirage.
Anayemkabidhi kadi ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Kaley Pandukizi na kushoto
ni Didi Vava.
Katibu wa CHADEMA, Liberatus Mwang;ombe (shoto) pamoja na Mwenyekiti wa
chama hicho tawi la DMV, Kaley Pandukizi wakipata picha ya pamoja na
Mwanachama mpya, Linda Expressl
Kutoka kushoto ni Helena Nyerere, Linda Express na Julia Nyerere
wakipata picha ya kumbukumbu
Ilikua ni furaha iliyoje kupata mwanacchama mpya, pichani wafurukutwa wa
CHADEMA wakipata picha ya pamoja.
Linda Express akicheka kwa furaha baada ya kupokea kadi ya uanachama
CHADEMA
Wafurukutwa wa CHADEMA wakishuhudia Linda Express akikamata kadi
Ombi (shoto) akipata picha ya pamoja na Selina
Linda Express akionyesha kadi "MOJA YANGU NA NYINGINE MUME WANGU" ndio
maneno aliyosikika akisema.
MBUNGE WA SINGIDA MJINI MH. ‘MO’ ATOA MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA SH. MILIONI 6 KWA SHULE 20 ZA JIMBO KWAKE.
Msaidizi wa
mbunge wa jimbo la Singida mjini na katibu mwenezi wa CCM manispaa ya
Singida Bw. Hassan Mazala (kulia), akimkabidhi Afisa wa idara wa shule
za sekondari jimbo la Singida mjini Bw. David Bulala jezi 300
zilizotolewa na mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam
Dewji. Wa kwanza kushoto ni katibu muhtasi wa Mbunge.
Msaidizi wa
mbunge wa jimbo la Singida mjini Bw. Hassan Mazala akizungumza kwenye
hafla ya kukabidhi jezi 300 kwa shule za sekondari za jimbo la Singida
mjini. Wa pili kulia ni Afisa wa shule za sekondari jimbo la Singida
mjini Bw. David Bulala na wa pili kushoto ni Katibu Muhtasi wa mbunge.
Baadhi ya
jezi zilizotolewa msaada na mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh.
Mohammed Gullam Dewji kwa shule 20 za sekondari jimboni humo.
Na Nathaniel Limu
Mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji ametoa msaada
wa vifaa vya michezo jezi jozi 300, zenye thamani ya zaidi ya shilingi
milioni sita kwa shule 20 za sekondari jimboni kwake.
Msaidizi wa mbunge huyo Bw. Hassan Mazala amesema hayo wakati
akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi jezi hizo, iliyofanyika kwenye
ofisi ya shirika lisilo la kiserikali la Saidia Singida yetu iliyopo
mjini Singida.
Amesema jezi hizo zilikuwa ni sehemu ya msaada ambao ulikuwa utumike
kwenye ligi maalum ya kombe la 'Mo' ambayo shule zote za sekondari jimbo
la Singida mjini zingeshiriki.
"Lakini baada ya ninyi kuandaa bajeti kubwa mno na wakati huo huo mbunge
wetu Dewji akikabiliwa na majukumu makubwa ya kutekeleza ahadi zake
nyingi, ligi hiyo tumeisitisha kwanza",amesema Mazala ambaye pia ni
katibu mwenezi wa CCM manispaa ya Singida.
Amesema kwa sababu ligi hiyo tarajiwa maandalizi yake bado, sasa maamuzi
ni kwamba jezi hizo zitumike katika maandalizi ya michezo ya shule za
sekondari (UMISETA).
Akifafanua zaidi, Mazala amesema wanafunzi na vijana walio nje ya shule,
wahamasishwe kupenda michezo ili pamoja na mambo mengine, waweze
kujijengea mazingira mazuri ya kujiajiri na kuajiriwa.
Kwa upande wake Afisa elimu taalum shule za sekondari manispaa ya
Singida Bw. David Bulala, alitumia fursa hiyo kumshukuru mbunge Dewji
kwa kuipunguzia ofisi yake makali ya gharama ya ununuzi wa vifaa vya
michezo.
This is the only time I've been to your website. Thanks for providing more information.
ReplyDeleteHere is my web-site ... IT Support Sydney