Wabunge wa Bunge la Afrika
Mashariki (EALA) leo wameapishwa rasmi kushika madaraka hayo huku
Tanzania ikiwa na Wawakilishi tisa katika Bunge hulo.
Wabunge
hao waliapa baada ya kupatikana Spika wa mpya wa Bunge hilo ambapo
safari hii ikiwa ni Uganda kushika Uongozi huo wa Juu wa Bunge na Mwana
Uchumi, Margareth Zziwa kuchukua nafasi hiyo.
Wabunge
wote wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Mashariki waliokula kiapo
hii leo ni pamoja na Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania kwenye Bunge
EALA, Alhaj Adam Omar Kimbisa na Katibu wake, Mh Shy-Rose
SaddrudinBhanji.
Wengine
ni Mhe. Anjela Charless Kizigha, Mh. Maryam Ussi Yahya,Mh.Nderkindo
Perpetua Kessy, Dkt Twaha Issa Taslima, Mhe. Abdullah Ali Hassan Mwinyi,
Mhe Bernard Musomi Murunyana Mhe. Charles Makongoro Nyerere na Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta anaeingia kwa wadhifa
wake wa Uwaziri.
Wabunge
hao wameapisha pamoja na wabunge wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda.
Shy- Rose Banji akitia saini nyaraka za kiapo.
Mhe. Samuel Sitta ni mwakilishi wa Tanzania.
Mhe.Abdullah Alli Hassan Mwinyi.
Mhe. Charles Makongoro Nyerere.
Mhe. Alhaji. Adam Kimbisa.
Dkt. Twaha Issa
Taslima.
Mhe.Nderkindo
Perpetua Kessy.
Mhe. Bernard Musomi
Murunyana.
Mhe. Anjela Charless
Kizigha, akila kiapo. Picha na FATHER KIDEVU
No comments:
Post a Comment