Kuanzia leo, taswira za vipindi vya luninga nchini Tanzania haitokuwa kama ile ambayo wengi wetu tumeizoea. Kuna kitu kipya na cha aina yake.Ni Talk Show inayokwenda kwa jina The Mboni Show ambayo mwenyeji au host wake ni mwanadada Mboni Masimba.
The Mboni Show, kitakuwa kinarushwa kila siku ya Alhamisi,Saa 3 Kamili Usiku Mpaka Saa 4 na kisha marudio yake yatakuwa yanafanyika Saa 7 Mchana na Saa 10 jioni siku ya Jumamosi. Kwa maana hiyo ni kipindi ambacho,bila shaka, kitakufanya usibanduke hapo utakapokuwa ukikitazamia kwa muda wa takribani saa 1. Yote hayo ni kupitia kituo cha televisheni cha EATV(East Africa Television).
Lakini Mboni Masimba ni nani? Kipindi chake kitahusu nini na kitakuwa na tofauti gani kutoka katika vipindi vingine kadhaa vilivyoko katika stesheni mbalimbali za luninga? Ili kupata majibu kwa maswali hayo na mengine,nilimtafuta Mboni Mashimba. Haya hapa ni mazungumzo yetu;
BC: Mboni, Karibu sana ndani ya BC. Mambo vipi?
MM: Mambo poa tu Jeff za kwako?
BC: Za kwangu nzuri Mboni. Asante kwa kukubali kufanya nami mazungumzo haya. Kwa kuanzia tu,Jina lako ni la kipekee kidogo…Mboni. Lina maana gani jina lako? Wazazi waliwahi kukwambia kwanini walikuita Mboni?
MM: Yeah ni kweli…jina langu ni la kipekee. Mimi ni Mboni…ile mboni ya Jicho. Kama unavyojua, mtu huwezi kuchezea Mboni ya jicho yako. Ukifanya hivyo utakuwa unajitafutia balaa. Mboni ni kitu cha kuangaliwa sana kwa sababu kipo very sensitive. Mama yangu aliniambia kwamba waliamua kuniita Mboni kwa sababu ni kitu cha thamani.Kwa maana hiyo nina thamani kubwa kwao na hususani ukizingatia kwamba mimi ni mtoto wa mwisho kwa mama yangu… Ha ha ha haaaaa
BC: Mara nyingi tunapokuwa watoto huwa tuna ndoto kibao za kuja kuwa watu fulani au kuwa kama fulani na fulani. Unakumbuka mambo gani muhimu wakati wa utoto wako. Na je unachokifanya hivi leo ni ndoto yako ya toka utotoni au la?
MM: Kwa kusema ukweli ndoto yangu toka nikiwa mdogo ilikuwa ni kupenda kuja kuwa mfanyabiashara mkubwa mwenye hela nyiiingi sana. Na pia nilikuwa natamani sana siku moja niwe Mbunge au Waziri. Kuwa na Talk Show haikuwa ndoto yangu hapo awali.Lakini kama unavyojua,maisha huenda yakibadilika na kadri mtu unavyokuwa na fikra tofauti nazo humjia mtu. Na lazima wakati fulani tukubaliane na ukweli kwamba sio kila ndoto inaweza kuja kweli. Hivyo basi, ni muhimu kwenda na wakati na jinsi dunia inavyokwenda na pia kutumia nafasi zinazojitokeza.
BC: Kwa kiasi kikubwa hivi leo wewe ni msichana maarufu nchini Tanzania. Lakini kuna watu ambao wanasema hawaelewi au hawajui chanzo hasa cha umaarufu wako. Wewe binafsi unadhani au unauelezeaje umaarufu wako.Nini chanzo?
MM: Binafsi naweza hisi labda umaarufu ulianzia niliposhiriki shindano la ulimwende la Miss Mbeya na Miss Southern Highland mwaka 2000 na hatimaye kushiriki Miss Tanzania mwaka huo huo.Lakini kama hiyo sio sababu basi naweza kusema labda ni kutokana na jinsi nilivyo mtu wa watu.Mara nyingi nimekuwa mstari wa mbele katika kujitolea kwa wenzangu,watanzania wenzangu kwa chochote kile ambacho ninakuwa na uwezo nacho. Isitoshe mimi ni mtu ambaye napenda sana kujichanganya na watu wa rika zote bila kubagua. Anyway, I was Born to Be a STAR ha ha ha haaaa
BC: Naam, sasa tuongelee kitu ambacho umekianzisha hivi karibuni. The Mboni Show. Hongera sana kwa hatua hiyo.Ilikuwaje wazo la kuanzisha The Mboni Show likakujia? Ni wazo binafsi au ushauri uliopewa na mtu?
MM: Naweza kusema ni mchanganyiko wa ushauri wa watu na instincts zangu mwenyewe. Sema kuna rafiki zangu kadhaa walianza kuniambia kama miaka minne iliyopita. Sikuchukulia maanani sana.Then mwaka 2010 nikiwa na rafiki yangu mmoja tunakula zetu mihogo pale Coco Beach kwa jamaa mmoja muuza mihogo maarufu kwa jina la ITV, akanishawishi tena kuhusu suala hili. Then nkaanza kutake serious. Nakumbuka aliniambia hivi wewe hujiulizi kwanini mara kwa mara unaitwa kwenye tv interviews na katika most of then ukienda huwa baadae unapata reviews nzuri? Basi kuanzia hapo ndio nkaweka msisitizo zaidi katika Talk show.Matokeo yake ndio hapa tulipo hivi sasa.
Stage ya The Mboni Show
BC: Katika pitapita yangu ya mitandaoni nimesoma mahali kwamba Oprah ni miongoni mwa wanawake wanaokuvutia sana na yeye ni sababu mojawapo ya w ewe kuanzisha The Mboni Show ikiwa kama hatua mojawapo ya kufanya kile ambacho amekuwa akikifanya. Kuna ukweli wowote katika hilo?MM: Ni ukweli kabisa kwamba Oprah Winfrey ananivutia kupita kiasi. Pamoja na hayo show yangu haitokuwa ki-Oprah moja kwa moja. Sitaki na wala siwezi kumuiga kwa kila kitu. Ntakachofanya mimi ni kuchukua yale ambayo naweza kuyachukua na hususani kwa kuzingatia mazingira ya Tanzania zaidi. The Mboni Show ni show ya kitanzania kwa ajili ya watanzania.
BC: Katika maelezo ya awali ya The Mboni Show umeeleza kwamba malengo ya show yako ni kuelimisha, kuhamasisha na kusaidia jamii ya watanzania. Mmejipanga vipi kufikia malengo hayo?
MM: Yaani Jeff you will be Suprised .Wewe subiri tu utajionea.Lakini ki-ukweli The Mboni Show imejipanga vilivyo. Nawaambia The Mboni Show ndio kimbilio la Watanzania na mwokozi wao ha ha ha ha
BC: Mlolongo wa kuanzisha TV show ni mrefu na bila shaka umepambana na vikwazo kadhaa mpaka kufikia hatua hii. Unaweza kunieleza kidogo kuhusu vikwazo ulivyopitia na kitu gani kilikuwa kinakupa msukumo kwamba endelea tu usikate tamaa?
MM: Jeff sio kitu rahisi kama watu wanavyofikiria. Mimi na timu yangu tumeanza production since April last year na imagine ndio kwanza tumemaliza juzi juzi.Ni wazi kwamba katika kutimiza lengo au azma hii nimepitia vikwazo vingi ambavyo kwa kweli nisingesimama imara ningeweza kabisa kukata tamaa. Lakini mwisho ya yote namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunisaidia mpaka kufika hapa.
Kwa upande wa kitu ambacho kilikuwa kinanipa msukumo naweza kusema ni asili yangu ya kuwa mvumilivu na mbishi sana ninapotaka la kwangu.Hizo ndizo silaha zangu; uvumilivu na ubishi wenye manufaa. Vikwazo vilikuwa vingi sana ingawa sitopenda kuvitaja.Kwa ufupi nawaambia sio kitu kirahisi hata kidogo, ni kukomaaa tu mpaka kieleweke.
BC: Tunaposikia mtu anaanzisha kipindi cha televisheni kuna maswali kadhaa yanakuja. Je kitakuwa ni kipindi cha kurekodiwa ndani ya studio maalumu au kitakuwa kipindi cha kurekodiwa nje ya studio kwa maana ya mtaani nk. Kwa upande wenu format ya production ya The Mboni Show imekaaje?
MM: Kwa upande wetu tuna sehemu maalum ya kurekodia kama hii session ya kwanza vipindi vyote tulirekodia pale Serena( zamani ilikuwa ikiitwa Movenpick). Nawashukuru sana Serena kwa mchango wao katika kufanikisha hili. Next session itakuwa the same japo huwa tunatoka kidogo na kurekodi nje. Kuna mtu ambaye tumerekodi naye nje na hivi karibuni tunapanga kuingia mtaani. The Mboni Show ni kwa ajili yenu watanzania. Popote tutawafuata.
BC: Upo ukweli kwamba Hosts wengi wa TV show huwa yawabidi wawe na tabia ya kujisomea sana ili kupata mawazo na mitazamo mipya kila mara na kwenda na wakati. Je, na wewe pia una hulka hiyo au umejipanga namna gani katika kuhakikisha kwamba sio tu unakwenda na wakati bali unapata ideas mpya mpya za show nk?
MM: Kama nilivyogusia hapo mwanzo, siri yangu kubwa ni kuangalia kwa makini show za wengine zinafanywaje. Namuangalia mtu kama Oprah,Tyra,Monique,Hellen etc ili kupata mtazamo tofauti na ili niweze kuboresha show yangu kila mara. Sidhani kama ni lazima sana kusoma sana vitabu kwa sababu inategemea na aina ya show uliyonayo au unayoifanya.
BC: Mbali na hii venture mpya ya kuwa Host wa TV show, wewe ni mjasiriamali. Siku hizi, kama tunavyoona, wanawake wengi zaidi nao wanaingia kwenye ujasiriamali. Una ushauri gani kwa wanawake wenzio kuhusiana na ujasiriamali?
MM: Kwanza lazima ujue hiki kitu ” Fanya kitu ambacho unakipenda na unakiweza. Wanawake wengi tunakurupuka kwenye ujasiriamali na wakati hatuuwezi. Watu wanafanya kama fashion. Let’s say mimi napenda kuwa na Boutique kwa sababu napenda fashion na ninaimudu.Haya sasa nina talk show kwa sababu naipenda na ninaimudu. Kwa hiyo wanawake wenzangu, tujaribu kufanya kitu ambacho tunakipenda na kukimudu. Ni rahisi zaidi kufanikiwa ukiwa na hayo mambo mawili. Mapenzi kwa kitu unachokifanya au kutaka kukifanya na uwezo wa kukifanya.
BC: Mwisho una ujumbe gani mahususi kwa watanzania? Na pia kwanini mtu achague kuangalia The Mboni Show badala ya show zingine lukuki kwenye luninga?
MM: Ujumbe kwa watanzania wenzangu “Tupende vya kwetu, tuthamini vya kwetu, Tupendane na tushirikane. Kama unaona una connection na wewe huna uwezo nao ila kuna mwingine anaweza basi msaidie na sio kubaniana na kuoneana vijiba vya roho bila sababu za msingi.. Na pia tupende kusifiana. Mwenzako kafanya kizur basi mpe hongera zake na kama kakosea basi muelekeze( muongoze).
Ha ha ha ha Trust me The Mboni show iko kitofaut kabisa na zile tulizozizoea. Kwenye The Mboni show unapata kila kitu.Full package ha ha ha ha.
Kwa mengi zaidi unaweza kutembelea tovuti rasmi ya The Mboni Show katika www.thembonishow.com.
Read more: UJIO WA THE MBONI SHOW: MAHOJIANO NA HOST WAKE,MBONI MASIMBA - BongoCelebrity
No comments:
Post a Comment