Friday, June 22, 2012

MANJI A APIGA MAGOTI KWA WANACHAMA WA YANGA, ATUA JANGWANI KUFANYIWA USAILI

Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji, akizungumza jambo jambo na mmoja wa wa wanachama wa klabu hiyo, Rukia Mohamed, wakati alipofika Makao Makuu ya klabu hiyo iliyopo mitaa ya Jangwani jijini Dar es Salaam leo,  ambapo alifika kwa ajili ya kufanyiwa usaili kwa ajili ya uchaguzi mdogo utakaofanyika Julai 15, mwaka huu.

Beki wa zamani wa Klabu ya Simba, aliyekuwa na ndoto lukuki ya siku moja kuvaa jezi ya rangi ya Njano na Kijani na kuichezea Klabu ya Yanga, Kelvin Yondan, (wa Pili kushoto), aliyesajiliwa hivi karibuni akishiriki na wachezaji wenzake wakati akikaribishwa na wachezaji hao alipofika kwa mara ya kwanza kushiriki mazoezi ya timu hiyo, leo yaliyofanyika  Uwanja wa Kaunda Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment