Irene Isaka, Mkurugenzi wa SSRA
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUSITISHWA KWAFAO LA KUJITOA |
Mamlaka
ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya
Hifadhi ya Jamii (SSRA), inapenda
kutoa ufafanuzi
juu ya mafao ya kujitoa. Ufanunuzi huu unakwenda
sambamba na taarifa mbalimbali ambazo
zimekuwa zikitolewa na vyombo vya
habari na
kuleta mkanganyiko miongoni mwa Wanachama na
Wadau wa Sekta ya
Hifadhi ya Jamii.
Kufuatia hali hiyo, Mamlaka inatoa ufafanuzi
ufuatao:
- Marekebisho
kuhusu kusitisha fao la kujitoa
yamefanyika ili kutimiza lengo na
madhumuni ya
Hifadhi ya Jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa
mwanachama
anapostaafu anapata mafao bora
yatakayomwezesha kumudu hali ya maisha
uzeeni.
- Ni
kweli kuwa Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii pamoja na Sheria ya
Mamlaka zimefanyiwa
marekebisho. Mchakato wa marekebisho hayo
ulihusisha
wadau kwa kuzingatia utatu yaani
wawakilishi kutoka Vyama vya
Wafanyakazi,
Chama cha waajiri pamoja na Serikali.
- Kwa
kutambua tofauti ya ajira, tofauti ya
mazingira ya kazi, tofauti ya
sababu za ukomo wa
ajira, na umuhimu wa Mwanachama kunufaika na
michango
yake wakati angali katika ajira
, Mamlaka inaendelea na mchakato wa
kuandaa
miongozo na kanuni za mafao ambazo lengo lake
ni kuboresha
maslahi ya Wanachama. Miongozo
na kanuni hizo zitajadiliwa na Wadau
wakiwemo
Wafanyakazi, Waajiri na Serikali kabla ya kuanza
kutumika.
- Kufuatia
kuanza kutumika kwa Sheria hiyo
maombi mapya ya kujitoa yamesitishwa
kwa
kipindi cha miezi sita hadi pale miongozo
itakapotolewa ili
kuiwezesha Mamlaka na Mifuko
ya Hifadhi ya Jamii kutoa elimu kwa Wadau.
- Tangazo hili halitowahusu Wanachama
waliojitoa kabla ya tarehe 20/07/2012.
- Mamlaka
inakanusha vikali kwamba, sitisho la
fao la kujitoa si kwa sababu za
Kiserikali au kwa
sababu mifuko imefilisika. Tunapenda
kuwahakikishia
kwamba Mifuko yote ipo thabiti
na michango yote ya Wanachama ipo salama.
- Hivyo,
Mamlaka inawaomba Wanachama na
Wadau wote wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
kuwa na
utulivu wakati mchakato huu ukiendelea kwa
lengo la kulinda na
kutetea maslahi ya
Mwanachama.
Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano na
Uhamasishaji
SSRA-Makao Makuu
No comments:
Post a Comment