Thursday, September 13, 2012

PICHA ZA JINSI ASKARI MTUHUMIWA WA MAUAJI YA MWANDISHI ALIVYOFIKISHWA MAHAKAMANI IRINGA.wakati wote alikua amefichwa hivi hivyo hata sura haikuonekana kwenye picha yoyote.
Kamanda wa polisi Iringa Michael Kamuhanda amethibitisha kwamba askari polisi ambae anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kukusudia ya mwandishi wa habari Daudi Mwangosi amefikishwa mahakamani Iringa september 12 2012.
Askari mwenyewe ni mwenye namba G2573 na jina lake ni Pasificus Cleophace Simoni mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa FFU Iringa.
Mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa mahakama ya hakimu Mfawidhi ya Wilaya Dyness Lyimo mtuhumumiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haiwezi kusikiliza kesi za mauaji.
.
Kwenye kesi za jinai sheria kifungu cha 196 iliyofanyiwa marejeo 2002 inakatazwa mtuhumiwa wa mauaji ya kukusudia kupewa dhamana ambapo mtuhumiwa amerudishwa mahabusu kutokana na kesi yake kukosa dhamana kisheria na kesi hiyo imeahirishwa hadi 26 Septemba mwaka huu itakapotajwa tena.
Kamanda Michael Kamuhanda amesema “ni kosa kama makosa mengine huwa yanatokea katika kazi, uchunguzi umekamilika na mtuhumiwa amefikishwa Mahakamani”
Hili ndio gari lililombeba mtuhumiwa.
siku ya tukio (picha zote zimepigwa na Francis Godwin)