Wagonjwa na watu wenye wagonjwa
hospitalini nchini Kenya sasa hivi wako kwenye hofu kutokana na
kutangazwa kuanza tena kwa mgomo wa Madaktari baada ya serikali kusema
haitobadilisha chochote kwenye mishahara ya madaktari.
September 13 2012 Madaktari
wote wa hospitali za Serikali Kenya wanatarajia kuanza kugoma kwa sababu
serikali haijafanya kama wanavyotaka, yani kuongezewa mishahara.
Katika vichwa mbalimbali vya
habari nchini Kenya Mtangazaji William Tuva wa Citizen Radio na Citizen
Tv ameripoti pia kwamba baada ya vurugu kuendelea kati ya makabila ya
Waorma na Wapokomo kwenye wilaya ya Tana River ambapo inaaminika zaidi
ya watu 100 wamefariki dunia wakiwemo Polisi, Mbunge wa Galole ambae ni
Naibu Waziri Godana amekamatwa na polisi na kupelekwa Mahakamani
akidaiwa kuwa mmoja ya watu wanaohusika na uchochezi wa hizo vurugu,
baadae aliachiwa kwa dhamana ya shilingi laki nne za Kenya.
Vurugu za sasa kwenye wilaya ya
Tana River zimehusisha watoto pia kuuwawa kikatili na nyumba kuchomwa
ambapo wataalamu wa mambo wanasema vurugu hizi zinahusika na siasa, yani
kuna wanasiasa wanachochea kwa sababu uchaguzi mkuu unakaribia.
Kwenye sentensi nyingine
William Tuva ameamplfy kuhusu mlipuko uliotokea Mogadishu Somalia kwenye
hoteli aliyokuwemo rais mpya wa Somalia pamoja na waziri wa mambo ya
nje wa Kenya Sam Ongeri lakini hao viongozi wote wamenusurika,
waliopoteza maisha ni watu wengine saba.
Waziri huyo wa mambo ya nje alikwenda Somalia kumwakilisha Rais Mwai Kibaki kutoa pongezi kwa rais mpya wa Somalia
No comments:
Post a Comment