Tuesday, October 9, 2012

IBADA YA MZEE MWAKASEKELE BABA WA ADELA YA FANA Ibada kwa ajili ya Mzee Mwakasekele baba yake na Adela aliyefariki  Tanzania September 26  na kuzikwa september 28 ilifanyika Jumapili October 7, 2012 Brooklyn, New York na kuhudhuliwa na Ndugu, jamaa na marafiki kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo,Boston, DC, Houston na vitongoji vya jiraniil Ibada  iliandaliwa na Adela ambae ni Mtoto wa marehemu anaehishi Brooklyn, NY kwa kushirikiana na ndugu pamoja na marafiki zake. Ibada hiyo iliongonzwa na Mchungaji mama Butiku. kutokana na watu walivyo jitokeza na jinsi walivyoonyesha moyo wa upendo kwake kutoka siku ya kwanza alivyopata taarifa ya msiba hadi siku ya Ibada Adela alifarijika sana. Viongozi wa jumuiya hapa New York walikuwa pamoja. Adela amewashukuru watu wote kwa moyo wa upendo walimuonyesha kwa kipindi hiki kigumu kwake kwa kumpoteza baba yake mzazi.

 Hapa Mchungaji Mama Butiku akiongoza Ibada hiyo iliyokuwa imefanyiko Roosevelt Island,NY 

 Adela akionekana mwenye majonzi akitoa shukurani zake kwa watu walio jitokeza katika Misa hiyo
Dada yake Adela anaeitwa Sophia kutoka DC akionekana mwenye majonzi akitoa shukurani zake kwa watu walio jitokeza katika Ibada hiyo
Mzee Seruhere afisa wa ubalozi New York akifikisha ujumbe kwa mfiwa kwa niaba ya Mhe. Balozi Manongi
Mueka hazina wa jumuiya ya NY Mzee Temba akiandika jina kitabu cha rambirambi na kulia ni Ismahan aliekuwa amepewa jukumu la kusimamia kitabu hicho.
Adela akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wenzie waliokuja kumpa support 
Dada yake Adela akiwa na marafiki zake kutoka DC Taji mfanyakazi wa ubalozi Washington, DC na Henry ambae ni Dr  waliokuja maalum kwenye ibada hiyo.
Kwa picha zaidi Bofya read more


Add caption