Thursday, October 4, 2012

MELI YENYE KUTOA HUDUMA YA UTOA MIMBA STOP KUTIA NANGA PWANI YA MOROCCO
Meli moja ya Uholanzi iliyokuwa ikielekea katika pwani ya Morocco kutoa huduma ya utoaji mimba kwa wanawake imezuiliwa kuingia bandarani kwa mujibu wa wanaharakati walioituma nchini humo. 

Kundi la wanaharakati hao wanawake linasema kuwa bandari ya Smir imefungwa kabisa na meli za kivita zinalinda doria eneo la bandari hiyo.

 Hapo jana Morocco ilisema kuwa meli hiyo haijapewa mualiko na mamlaka zinazotambuliwa nchini humo na hivyo ilikuwa ikifanya shughuli hiyo kinyume cha sheria. Sheria za Morocco zinakataza utoaji mimba isipokuwa tu iwapo maisha ya mwanamke mjamzito yako hatarini. 

 Ibtissame Lachgar, ambaye ni mmoja wa wanaharakati wanaotetea haki ya utoaji mimba amesema wanawake wengi wanalazimika kufanya utoaji mimba kwa njia zisizo rasmi ambazo ni hatari.