Tuesday, January 8, 2013

ABIRIA 'MZUNGU' AONYESHA UUNGWANA KWA DEREVA WAKE WA BAJAJI


Abiria wa kike mwenye asili ya kigeni 'Mzungu', akimsaidia dereva wake wa Bajaji, ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, baada ya usafiri wao wa Bajaji kupata pancha eneo la Lugalo Jeshini Barabara ya Bagamoyo, jijini Dar es Salaam, leo asubuhi. Abiria huyo mwanamama alionyesha ushirikiano wa hali ya juu huku akimsaidia dereve huyo kuinua Bajaji hiyo upande mmoja ili waweze kufungua tairi bovu na kubadili na kuendelea na safari yao na kuwaacha hoi watu wote waliokuwa wakiwaona katika harakati zao. Je angekuwa ni abiria mwanamke wa 'Kibongo' angeweza kutoa msaada huu wa hali na mali kwa kumsaidia dereva wake au ndo kwanza angesimamisha Bajaji nyingine na kusepa zake??? 
''Hadi kieleweke'' Abiria mzungu, akimsaidia dereva wakekuinua Bajaji ili kubadili tairi.....
''Moja, Mbili, Tatuuuu, Haya twendee........Imeinuka kazi sasa kufungua tairi.
Shuguli ilianza hivi Mdada mzungu akiwa na vijitambaa mkononi kwa ajili ya kushikia bodi la Bajaji kuepuka kuumia mikono.