Thursday, January 31, 2013

JENEZA LAKUTWA SOKO KUU MWANZA KIONGOZI WA WAFANYABIASHARA SOKONI HAPO NDIYE MUHUSIKA.


Katika hali isiyokuwa ya kawaida kiongozi mmoja wa ngazi za juu wa soko kuu la jijini Mwanza leo amezuwa sokomoko na taharuki kwa wafanyabiashara wa soko hilo mara baada ya kukutwa na jeneza la kusafirishia maiti katika sehemu yake ya biashara tena juu ya magunia ya viazi sokoni hapo.


Aliyezua taharuki hilo ni mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko kuu la jijini Mwanza ambaye pia ni mfanyabiashara wa viazi wa soko hilo Bw. Hamad Nchola ambaye alikuwa hakuwa na majibu ya moja kwa moja balimajibu mafupi mafupi yasiyoridhisha wakati akihojiwa na waandishi wa habari.

Baadhi ya wafanyabiashara na wanunuzi wakijadiliana juu ya kuwepo kwa jeneza hilo katika eneo la banda la biashara la mwenyekiti soko kuu la Mwanza.


Jeneza juu ya magunia ya viazi ndani ya banda la biashara la mwenyekiti.


Bw. Hamad Nchola ambaye ni mwenyekiti wa wafanyabiashara soko kuu la Mwanza aliyezua balaa. 


Naye Mwenyekiti huyo akijitetea kuhusu sakata hilo amesema kuwa aliamua kufanya uamuzi huo wa kuhifadhi jeneza hilo sokoni hapo kwenye sehemu yake ya biashara mara baada ya kulichukuwa kutoka msikitini akisubiri usafiri kulipeleka hospitali ya Rufaa ya Bugando kuuchukuwa mwili wa mke wa mfanyabiashara mwenzake sokoni hapo ambao ulipaswa kusafirishwa kuelekea wilayani Magu kwa mazishi.


Alipohojiwa kwa nini asingeliacha jeneza hilo msikitini au kulipeleka nyumbani kusubiri muda muafaka badala ya kulihifadhi sokoni hapo ambako kunatambulika kuwa ni sehemu mahususi kwaajili ya biashara ya mazao na chakula pamoja na kuwa na watu wenye imani tofauti, mfanyabiashara huyo alisema aliamua kufanya hivyo kwakuwa hakuona shida na alifanya hivyo kama wafanyabiasha wengine na kwamba inshu hiyo imekuwa kubwa kwa kuwa yeye ni kiongozi.Kisha akaongeza kuwa kufanya hivyo siyo tatizo na jeneza hilo ni mbao tu na siyo kitu cha kustaajabisha na aliamua kulihifadhi eneo la biashara yake kwa kuhofia kuwa lingenyeshewa na mvua.

Baadhi ya wafanyabiashara na wanunuzi wakichungulia eneo la banda la biashara la mwenyekiti ambapo kuna jeneza hilo.


Pamoja na kuwa na kigugumizi kujibu kuhusu muda alilolileta jeneza hilo sokoni hapo kwamujibu wa mmoja wa walinzi ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa jeneza hilo liliingia sokoni hapo mapema alfajiri wakati hakukuwa na wafanyabiashara sokoni hapo hali ambayo ilimshitua na mlinzi huyo akashindwa kuhoji kwakuwa ni mfanyabisha huyo ni bosi wake.


Hata hivyo baadhi ya wafanyabiashara waislamu wamepinga vikali kuwa jeneza hilo si mali ya misikiti kwa kuwa waumini hao hawatumii masanduku ya miundo hiyo hususani hilo lenye tundu la kuagia, zaidi ya kutumia majeneza yenye mikono minne hivyo wamemtaka kiongozi huyo kuhojiwa zaidi juu ya sakata hilo.Vijana wakifanya mchakato kuliondoa jeneza hilosokoni hapo toka kwenye banda la biashara la mwenyekiti.Hatimaye Jeneza hilo liliondoshwa sokoni hapo na vijana waliolibeba msobemsobe kwenye majira ya saa 4 asubuhi ya leo lisijulikane lilipoelekea.