Wednesday, January 30, 2013

KIPAJI CHA KUKATA NYONGA CHA MPA NEEMA SNURA KAYASEMA HAYO


MSANII wa filamu na muziki Snura Mushi ‘Snura’, anayetamba kwa mauno, ameeleza kuwa mwaka huu anaamini ni mwaka wake wa kukimbiza kutokana na mapokezi makubwa anayoendelea kuyapata kutoka kwa mashabiki wake hasa kwenye show zake.
Snura alizungumza na mwandishi wa DarTalk, ambapo alisema kuwa muziki wake umeedelea kumweka juu, na anaamini ujio wake wa mwaka huu kila msanii anayemfuata nyuma yake atasubiri kwani anajua kile anachokifanya kwa akili ya mashabiki wake.
Hata hivyo alisema kuwa anatarajia kuzindua rasmi video yake mpya ya ‘Majanga’ kwenye usiku wa Viuno Show ndani ya New Maisha Club Jumapili hii ambapo pia atasindikizwa na wakali wengine kibao.
“Nafanya muziki na filamu na huwezi amini mashabiki wangu wamekuwa wakipokea kwa shangwe sana pale napoenda kufanya show, naamini huu mwaka kwangu utakuwa na mafanikio makubwa sana tofauti na nyuma,” alisema. Toa Maoni yako Hapa chini