Wednesday, January 30, 2013

MUNGU NI MWEMA TOUCHING STORY
Hili ni simulizi la kweli linalomhusu mwanamke mmoja ambaye alikuwa ni kahaba wa makahaba.....Mwanamke huyu alijitambua vyema na kukiri ndani ya nafsi yake kuwa hawezi kuolewa na maname yoyote yule maana jamii yote ilikuwa inamtambua kwa uchangudoa wake......
Kwa hiyo , ili kurahisisha mambo na kuifanya biashara yake iimarike, mwanadada huyu aliamua kwenda hospitali kukitoa kizazi chake.Hakutaka tena usumbufu wa kutoa mimba au kufikiria kondomu......

Tangu wakati ule biashara yake iliimarika na wateja walizidi kumiminika.Baada ya miaka kadhaa, Upako wa mwenyezi mungu ulimfikia kupitia kwa mtumishi mmoja wa mungu ambaye alifanikiwa kumfanya aokoke na kuwa mtumishi mzuri kanisani.....

Siku moja, mchungaji mmoja alimwita na kumwambia kuwa:
"Dada yangu, Mwenyezi mungu amenena na mimi na kunifunulia kuwa wewe ndo mke wangu wa ndoa, hivyo naomba tuoane.."

Mwanamke huyu alitabasamu na kusema:
"Kaka yangu, Mungu hajakwambia lolote, lasivyo, utakuwa hujamsikia vizuri.Naomba uniache tu maana sina mpango wowote wa kuolewa"

Yule mchungaji aliendelea kushikilia msimamo wake na kudai kuwa :

"Mungu amenifunulia,wewe ndo mke wangu" 

Mwanamke huyu aliendelea kuyapuuza maneno hayo na ndipo sakata hilo lilipomfikia Askofu wa kanisa hilo.....

Wakiwa mbele ya mchungaji,Mwanamke huyu alifunguka kwa uwazi mbele ya askofu na kudai kuwa kabla ya kuokoka yeye alikuwa ni kahaba wa makahaba....

Askofu naye alifunguka na kudai kuwa :"Sioni sababu ya kuumiza kichwa kwa mambo yaliyopita.Mungu humsamehe mwanadamu kwa kuzifuta dhambi zake zote za nyuma na kumfanya awe mpya..!!!"

Mwanamke huyu alifunguka tena na kudai kuwa:
"Baba askofu, mimi nilishatoa kizazi changu wakati nikiwa kahaba, kwa hiyo sitaweza kuzaa tena"
Askofu aliishiwa pumzi baada ya kusikia hivyo.Hakuweza tena kusema kuhusu kusahau ya nyuma.Ilibidi amgeukie yule mchungaji na kumwamba: 

"Vipi, bado kuna maono yoyote toka kwa mwenyezi mungu?" 
Mchungaji alijibu ,"Ndio, huyu ndo mke wangu.."
Askofu ilibidi awaombee kwa sala maalumu.Hatimaye ndoa ikafungwa......Baada ya miezi michache tu, huyu mwanamke alibeba mimba.Yeye pamoja na mumewe waliongozana pamoja kwenda hospitalini, tena kwa yule yule doctor aliyekitoa kile kizazi......

Daktari alipomuona alifurahi akidhani kuwa pengine mteja wake kamletea mteja mwingine.....Doctor hakuamini masikio yake baada ya kuambiwa kuwa huyu mwanamke ni mjamzito na amekuja kujiandikishaclinic....
Hakika Mungu ni Muweza wa yote....