Saturday, January 19, 2013

MKUTANO WA BARAZA LA BIASHARA LA ZANZIBAR ZBC

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua Mkutano wa Saba (7) wa Baraza la Biashara la Zanzibar ZBC,uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja,(kulia) Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abduhamid Yahaya Mzee,na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko,Nassor Ahmed Mazrui.
Baadhi ya watendaji wa Taasisi mbali mbali wakifuatilia kwa makini agenda za mkutano wa Saba ( 7) wa Baraza la Biashara la Zanzibar ZBC uliofanyika leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
Wajumbe wa Mkutano wa Saba wa Baraza la Biashara la Zanzibar,kutoka Taasisi na Makampuni mbali mbali ,wakifuatilia kwa makini taarifa na mada zilizotolewa katika mkutano huo,uliofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel,Mjini Unguja. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]