Tuesday, January 29, 2013

UONGOZI WA KOMBE LA MAPINDUZI, WAKUTANA NA RAIS IKULU ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Cheti cha Shukurani, Meneja wa Benki ya Watu wa Zanzibar Limited,(PBZ) Juma Amour, kwa Mchango wa Benki hiyo kufanikisha michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyomalizika hivi karibuni. Hafla fupi ya mazungumzo na kukabidhi vyeti kwa waandaaji hao ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar leo mchana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Cheti cha Shukurani Ibrahim Raza wa Kampuni ya Hassan & Sons.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Mapinduzi CUp na Wahisani waliochangia Kombe la Mapinduzi CUP,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza nao leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Mapinduzi CUP ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar,kupata kupata nasaha pamoja na kukabidhi vyeti vya Shukurani kwa wahisani waliochangia kufanikisha mashindano ya Kombe la Mapinduzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo na Wahisani waliochangia Kombe la Mapinduzi. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.