Thursday, January 24, 2013

WASIRA AKWAMA KUSURUHISHA MGOGORO WA KUCHINJA BAINA YA WAISLAMU NA WAKRISTU

Leo kutwa nzima Wasira alikuwa akikutana na pande mbili baina ya Waislamu na Wakristu kuhusu nani mwenye haki ya Kuchinja.

Wasira alianza kwa kuzungumza na viongozi wote kicha kuzungumza na Waislamu pekee na baadaye Wakristo, lakini katika majumuisho alipowakutanisha wote alieleza kwamba msimano wa serikali waendelee kuchinja Waislamu lakini na Wakristu wachinje majumbani kwao.

Uamuzi huo umepingwa na Wakristu na kusema suala la kuchinja Waislamu nyama ya Bucha lilikuwa ni ustarabu na siyo sheria hivyo kugomea maamuzi waziri Wasira wakieleza hata wakristu wanayo haki ya kuchinja.