Thursday, January 24, 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 23.01.2013.

KAMANDA DIWANI RPC MBEYA

WILAYA YA MBEYA VIJIJINI - AJALI YA GARI KUACHA NJIA KUGONGA NYUMBA NA KUSABABISHA KIFO
MNAMO TAREHE 22/01/2013 MAJIRA YA SAA 18:30 HRS HUKO MAENEO YA IMEZU KATIKA BARABARA YA MBEYA/IRINGA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA.. GARI NO T 905 AGX / T 844 ASK AINA YA SCANIA LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA ANUANI YAKE LILIACHA NJIA NA KUGONGA NYUMBA YA NDELE S/O KWIMBA , MIAKA 50,MSAFWA,MKULIMA NA MKAZI WA IMEZU NA KUSABABISHA KIFO CHAKE MAJIRA YA SAA 22:30 HRS WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA . DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI HIYO NA KULITELEKEZA GARI ENEO LA TUKIO. CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO NA JITIHADA ZA KUMTAFUTA DEREVA HUYO ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA NA TAHADHARI WAWAPO BARABARANI KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ZILIZOWEKWA ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA ALIKO DEREVA HUYO AZITOE ILI AKAMTWE VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.


WILAYA YA MBEYA MJINI - KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]


MNAMO TAREHE 22.01.2013 MAJIRA YA SAA 11:00HRS HUKO KATIKA KILABU CHA POMBE ZA KIENYEJI MAKETE {B} MWANJELWA JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA DAVID S/O EDWIN, MIAKA 38, KYUSA, MKULIMA KAZI WA MAKUNGULU AKIWA NA POMBE YA MOSHI UJAZO WA LITA 5 . MTUHUMIWA NI MUUZAJI, TARATIBU ZINAFANYWA ILI MTUHUMIWA AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.


WILAYA YA MBEYA MJINI - KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]


MNAMO TAREHE 22.01.2013 MAJIRA YA SAA 11:00HRS HUKO MWANJELWA JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA MARRY D/O MBUYA, MIAKA 62, KYUSA, MKULIMA KAZI WA KABWE AKIWA NA POMBE YA MOSHI UJAZO WA LITA 9. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZINAFANYWA ILI MTUHUMIWA AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.


WILAYA YA MBEYA MJINI - KUPATIKANA NA BHANGI.


MNAMO TAREHE 22.01.2013 MAJIRA YA SAA 11:45HRS HUKO ILOMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA LUGANO S/O KENEDY,MIAKA 28,MNGONI,MKULIMA KAZI WA ILOMBA AKIWA NA BHANGI KETE 40 SAWA NA GRAM 200 MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MVUTAJI WA BHANGI, TARATIBU ZINAFANYWA ILI MTUHUMIWA AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

Signed By,
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.