Tuesday, February 12, 2013

"JULIANA SHONZA NA MTELA MWAMPAMBA KARIBUNI CCM. CHAMA KINACHOJIPAMBANUA KWA UKWELI NA UWAZI. CHAMA KINACHOTOA UHURU WA MAWAZO NA FURSA KWA WOTE" - Nape NNauye


NAPE MOSES NNAUYE:
KARIBUNI SHONZA NA MWAMPAMBA.,Karibuni CCM...!Sasa imetimia kauli na maono ya walio wengi wenye busara na hekima ya kutazama mambo kwa weledi mkuu. Kwa yaliyokuwa yanaendelea Chadema yakiratibiwa na kupigiwa chapuo na BABU wa Chama hiko na watu wa kundi lake, sasa yamedhihiri kuwa yanakimaliza na kukizika moja kwa moja Chama hiko.Ni jambo la hatari kwa chama ambacho viongozi wake wana uwezo wa kukandamiza, kubaguza wenzao kwa namna wanavyojisikia bila kuzingatia mchango wao, hadhi yao na muruwa wao., wanaweza kufanya lolote kwa yeyote ndani ya Chama kwa kadri wanavyojisikia wao. Ni hatari kuwepo watu miongoni mwa jamii ambao Ubaguzi kwao ni Sera ya kujinadi kwa watu, ni hatari sana...!Shonza na Mwampamba wameiona hatari hiyo na vijana na wanachama wengine wa CHADEMA waione hatari hii ya kuongozwa na watu ambao hawajui nini maana ya kuwa kiongozi, hawajiheshimu wenyewe na hawaheshimu wengine, ni watu ambao maslahi binafis yanatangulia maslahi ya wengi, hawana uzalendo na wamekosa hata chembe ya Utaifa. Watu wanaohubiri chuki na kuhamasisha Utengano, watu ambao wamekosa mapenzi na Taifa lao kiasi cha kuwa tayari kufanya lolote ili kuhakikisha kuwa nchi hii haitabiriki na kuandika ripoti za uongo na uchochezi kwa mataifa makubwa na jumuiya za kimataifa kuwa TANZANIA si sehemu salama ya kuishi wala kuwekeza, ni wazandiki wasiolitakia mema Taifa hili.


Chadema kuna Viongozi ambao hawatendi haki baina yao kama viongozi lakini pia hawatendi haki kwa wanaowaongoza, wanaipinga na kuikataa kweli hata ikidhihiri mbele ya macho yao. Ni watu ambao hawaheshimu, hawasimamii na wanapuuza Katiba waliyojitungia wenyewe, hawako balanced katika maamuzi wala katika hukumu


Natoa ANGALIZO Kwa vijana ambao wanajitoa kuijenga na kuitetea CHADEMA umefika wakati sasa wa ninyi kuiona hatari hii ndani ya Chama hicho mnachokiamini na kutafuta Chama kingine ambacho hayo yanayowakuta chadema hayatowakuta., Karibuni CHAMA CHA MAPINDUZI.,Chama kinachodumisha mapinduzi na mageuzi ya kweli katika jamii.,Chama kinachotoa fursa kwa wanachama wake kusikilizwa na kuthaminiwa kwa michango yao na huduma yao kwa Chama.


Napenda kuchukua fursa hii kumtaka Zitto Kabwe kuiona hatari hii lakini pia kumkaribisha CCM, ambako michango yake itathaminiwa na wala hatobaguliwa na kunyanyaswa bali atathaminiwa na kuheshimika.

Nawapongeza JULIANA SHONZA na MTELA MWAMPAMBA kwa kuiona hatari iliyoko chadema na kuchukua uamuzi wa kujiunga CCM, naamini wataleta michango bora na mawazo yenye kujenga.

Kwa wale wafuata upepo na mashabiki wa siasa, hii ni fursa kwao kujikumbusha fasihi ya TOPAN kwenye MFALME JUHA aliposimuulia kisa cha BAKARI na WALII walipofika nchi ya kichaa ambayo mfalme wake alitoa tangazo la kila kitu ratili moja kwa pesa moja na WALII kumtaka BAKARI wahame nchi hiyo ila BAKARI aling’ang’ania kubaki na yaliyomkuta mnayajua…!Karibuni CCM.,Umoja wetu ndio ushindi wetu...!