Tuesday, February 12, 2013

MKATABA WA MAELEWANO WASAINIWA MKOANI KAGERA KUENDELEZA KITUO CHA KUWATUNZA WAZEE NA WTOTO YATIMA KIILIMA -BUKOBA

Katibu Tawala Mkoa Kagera wa Kwanza Kushoto Bw. Nassor Mnambila Pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya UOA-T na SAJAWAKA Kulia Wakijitayarisha Kuaini Mkataba wa Maelewano Katika Kuendeleza Kituo cha Kutunza Wazee na Watoto Yatima Kiilima
Katibu Tawala Mkoa Kagera Bw. Nassor Mnambila Akipena Mkono Peter B. Temalilwa Muwakilishi SAJAWAKA baada ya Kuweka saini Katika Mkataba wa Maelewano.
Katibu Tawala Mkoa Kagera Bw. Nassor Mnambila Akisaini Mkataba wa Maelewano Kati ya UOA-T na SAJAWAKA.

Wazee na watoto yatima wanaotunzwa katika kituo cha Kilima Halmashauri ya Wilaya Bukoba mkoani Kagera wapata ufadhili ili kuboreshewa mazingira wanayoishi pia na huduma zote wanazostahili kupata katika umri wa uzee na watoto yatima.



Ufadhili huo utapatikana baada ya Katibu Tawala Mkoa Kagera Bw. Nassor Mnambila kutiliana saini katika Mkataba wa Maelewano leo tarehe 12/02/2013 na mashirika mawili yasiyokuwa ya serikali kuhudumia kituo hicho kwa miaka mitano kwa pamoja yakishirikana na serikali.

Bw. Mnambila amesaini mkataba huo kwa niaba ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwasababu kituo hicho kipo chini ya wizara hiyo, isipokuwa serikali ya mkoa wa Kagera imehusika kusaini mkataba wa maelewano kwaajilia ya ufuatiliaji wa karibu katika kituo hicho.

Mashirika yaliyotiliana sahihi na serikali ya Mkoa ni UKIMWI Orphans Assistance (UOA), U.S.A, P.O.Box 29074 Washington, DC 20017 kupitia UKIMWI Orphans Assistance - Tanzania (UOA-T), P.O. Box 1074 Bukoba, shirika hilo litashirikiana na Saidia Jamii ya Wazee Kagera (SAJAWAKA) P.O.Box 603 Bukoba.

Katika mkataba huo wa maelewano mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yatahusika na kukarabati miundombinu ya kituo hicho cha Wazee na Watoto yatima ambayo ni pamoja na mabweni, bafu, nyumba za watumishi, jiko, stoo na bwalo la chakula na kuweka samani ndani ya majengo hayo.

Aidha pamoja na kushirikiana na mashirika hayo, serikali itaendelea kuhakikisha utulivu na amani katika kituo hicho. Pia serikali itaendelea kutoa huduma zilizokuwa zikitolewa hapo mwanzo kama mishahara ya watumishi wa kituo hicho na huduma nyingine kama chakula ilizokuwa ikizitoa tangu awali.

Matarajio ya Baadae, Serikali katika kuongeza ushirikiano wa kutoa huduma za kijamii kwa kushirikiana na Sekta binafsi (Public and Private Partnership, PPP) inatarajia kujenga dispensari katika kituo hicho ili kuhudumia wazee, watoto yatima pamoja na jamii ya Kilima.

Kuhakikisha kituo hicho kinajiendesha kwa kutegemea kilimo na kupata chakula cha kutosha kukidhi mahitaji ya kituo. Pia kukisaidia kituo hicho kunufaika na rasilimali zinazotarajiwa kupatikana katika kituo hicho.

Kituo cha Kiliima kinatarajiwa kufanywa kituo cha mafunzo kwa vitendi kwa wanafunzi wa elimu ya kijamii na Afya ambao watajifunza kwa vitendo kuwatunza wazee na watoto yatima na baadae kuajiliwa katika sehemu mbalimbali za Tanzania kuwatunza wazee na watoto.

Kituo cha Kiilima Kilianzishwa mwaka 1972 na serikali ya Tanzania chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwajili ya kuwatunza wazee na watoto yatima. Aidha Shirika la UOA-U.S.A/UOA-T, ni kati ya mashirika yasiyokuwa ya serikali na limefanya kazi mkoani Kagera kwa miaka 23, pia SAJAWAKA limefanya kazi mkoani Kagera kwa miaka 12.

Hili ni jengo Mojawapo Katika Kituo cha Kuwatunza Wazee na Watoto Yatima Liloezuliwa na Upepo na Kuwafanya Wazee wa Kiilima Kubakia na JengoMoja. 
Bibi Huyu ni Mmojawapo Kati ya Wazee Wanaotunzwa Kituoni Kiilima Katika Halmashauri ya Wilaya Bukoba.

No comments:

Post a Comment