Wednesday, February 13, 2013

KLABU MPYA YAZINDULIWA ARUSHA AFRIKA MASHARIKI NA KATI HAKUNA KAMA IYO USIPIME NI WORLD GARDENHuu ni muonekano wa jengo la world garden inavyoonekana kwa nje
apa ni geti kuu la kuingialia katika jengo la world garden ilipo mushono ndani ya jiji la Arusha
katikati mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa mulongo akiwasili kuzindua rasmi jengo hili la world garden
wadau mbalimbali walishiriki katika uzinduzi wa ukumbi huu wa world garden ambapo katika jengo hili kuna vitu mbalimbali ikiwemo ukumbi wa disco afrika mashariki na kati hakuna kama huu kwani ni mkubwa na pia ni mzuri kuliko yote
mkuu wa mkoa wa Arusha magesa mulongo akizindua jiwe la msingi katika jengo hilo


mkuu wa mkoa wa arusha kiwa na mkurugenzi mtendaji wakiwa wanakata utepe wa lango kuu la kuingialia katika jengo hilo
mkuu wa mkoa wa Arusha pamoja na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya world garden wakiwa wanatembelea jengo hilo mbara baada ya mkuu huyo kuzindua rasmi apa ni ngazi za kuingilia katika ukumbi wa disco

mkuu wa mkoa akiwa na vingozi wengine pamoja na wageni waalikwa wakiangalia jinsi jengo hilo lilivyo ndani hapa wapo ndani ya ukumbi wa disco
mkuu wa mkoa akiteta jambo na mkurugenzi mtendaji wa world garden


picha juu na chini maeneo mbalimbali ya ukumbi huo ikiwemo sehemu za kupumzikia ukiwa disco au klabu


hii ni kaunta ilikuwa bado aijawekwa vinjwaji lakini ndo muonekano wake huo


apa ndipo dj wanakaa kufanya mambo
huu ni ukumbi wa mikutano uliopo ndani ya jengo hilo la world garden usipime na usiache kutembelea kwa kesho ambapo ni siku ya wapendanao kutakuwa na disco zuri kutaka kwa madj wakali ambapo kiingilio kitakuwa ni shilingi elfu 15 tu 


Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo amewataka wananchi wa mkoa wa Arusha kuanza kuwekeza katika sekta mbalimbali ili kuweza kuweka mkoa wetu katika madhari na hadhi ya jiji

Aliyasema hayo jana wakati akifungua jengo jipya la mikutano pamoja na ukumbi wa disco lililopo jijini hapa lijulikanalo kwa jina la World garden lililopo katika kata ya mshono ndani ya jiji la Arusha

Alisema kuwa mkoa wa arusha kwa sasa umepandishwa hadhi na kuwa jiji hivyo ni wajibu wa wazawa kuwekeza katika mambo mbalimbali akitolea mfano kuwa mpaka sasa pamoja ya kuwa wananchi ni wengi na wageni ni wengi lakini mpaka sasa kuna sehemu super makerti moja tu kitu ambacho kinatia aibu kwa jiji kubwa kama hili

Alisema kuwa viwanja vipo vya kujengea sehemu hizo ni watu wa kuwekeza tu hivyo aliwasihi wawekezaji wajitokeze kwa wingi kuwekeza katika vitu mbalimbali ili kuweza kuwezesha jiji letu kuwa la kimataifa

Alibainisha kuwa wafanyabiashara wakubwa wamekuwa wanaogopa kwenda kuchukumikopo na kuwekeza katika vitu mbalimbali lakini aliwatoa hofu na kuwaambia kuwa mikopo ipo na ni haki ya kila mmoja kwenda kuchukuwa mkopo kwani nafasi zipo wazi na mikopo ipo ya kutosha huku akibainisha kuwa amna mfanyabishara yeyote mkubwa anafanya kitu pasipo kuchukuwa mkopo

Alipongeza uongozi wa kampuni ya world garden na kudai kuwa wameweza kupiga atua kubwa kwani kufungua kwao kwa jengo hilo litasaidia kwa kiasi kikubwa kwani vijana wengi watapata ajira kupitia jengo hilo kwani katika jengo hilo kuna vitu vingi kwama vile ukumbi wa disco watu wa usafi wa nje na mengine mengi ambapo watu wote wanaotakiw akufanya kazi huku ni watanzania vijana hivyo watakuwa wamesaidia vijana kupata ajira

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa World garden alisema kuwa wao kama kampuni yao inampango wa kutoa ajira kwa zaidi ya vijana 120 na pia alisema kuwa watajitaidi kuboresha vitu mbalimbali .


Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka akizungumza na kuzindua wimbo maalum wa NSSF uliotungwa na Wasanii hapa nchini wajiitao All Stars,mbele ya wadau waliohudhuria mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza leo Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.Kauli mbiu ya mkutano huo kwa mwaka huu ni Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike. 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akifafanua jambo kwa umakini mbele ya Wadau zaidi ya 1000 kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania, kwenye mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaondelea hivi sasa kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ni Sekta ya hifadhi ya Jamii Tanzania,Njia panda-Nini kifanyike.. 
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crenscentius Magori akifafanua jambo mapema leo asubuhi wakati mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza leo Februari 13,ukiendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Meneja wa kanda na anaeshughulikia Idara mbalimbali za serikali kutoka NSSF,Rehema Chuma akifafanua namna ya uendeshaji wa shirika hilo kwa wadau waliohudhuria mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza leo Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Sehemu ya Meza kuu ya mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Pichani juu ni wadau mbalimbali wakifuatilia mkutano
Pichani shoto ni Meneja Mahusiano wa PPF,Lulu Mengele na mdau mwingine wakifuatilia yanayojiri ndani ya mkutano huo unaoendelea hivi sasa.
Pichani shoto ni Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini (CHADEMA),Mh Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu akiwa sambamba na Mbunge wa Arumeru Mashariki,Mh Joshua Nasari (CHADEMA) na Wadau wengine wakifuatilia yanayojiri hivi sana kwenye mkutano wa NSSF.
Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali wakifuatilia yanayojiri ndani ya mkutano wa NSS unaoendelea hivi sana ndani ya ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha
Pichani shto ni Mbunge wa jimbo la Ludewa,Mkoani Njombe,Mh Deo Filikunjombe (CCM) akiwa na baadhi ya Wabunge Wenzake wanaohudhuria mkutano huo wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri ndani ya mkutano huo ambao umewakutanisha wadau zaidi ya 1000 kutoka sehemu mbalimbali jijini Arusha.
Mwenyekiti wa kikao cha awamu ya kwanza cha Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Bwa.Daudi Msangi akitoa utaratibu kwa Wanachama na wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano huo unaoendelea ,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha,kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crenscentius Magori mapema leo asubuhi kabla ya kuanza kwa mkutano wa shirika hilo.
Mmoja wa wajumbe wa NSSF,Peter Sumbi aliyekuwa akifanya kazi shirika la Wildlife Fund akitoa ushuhuda wake,namna alivyopata ajali na kufanikiwa kupata fao lake la ajali kazini kutoka kwa shirika la NSSF na hatimaye kufaidi matunda kupitia mfuko huo.
Pichani ni Mwenyekiti wa wasataafu wa TAZARA,Injinia Mwl.Sango akitoa ushuhuda wake kuhusiana na namna shirika la NSSF lilivyowasaidia wastaafu wa shirika la TAZARA,kupitia mfuko wa pensheni na fao la kujitoa.

Mgeni Rasmi katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd (wa tatu kulia) na Mkewe,Mama Asha Seif Idd (wa pili kushoto) wakiwasili kwenye hoteli ya Mount Meru,Jijini Arusha usiku huu tayari kwa ufunguzi wa Mkutano huo utakaoanza kufanyika kuanzia Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.Wengine pichani ni Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka (katikati),Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Dkt. Makongoro Mahanga (wa pili kulia),Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF,Ndg. Aboubakar Rajab (nyuma ya Waziri Kabaka) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau (kulia).
Mgeni Rasmi katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd akisoma hotuba yake wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) utakaoanza kufanyika kuanzia Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka akisoma hotuba yake usiku huu wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) utakaoanza kufanyika kuanzia Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akizungumza machache usiku huu wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) utakaoanza kufanyika kuanzia Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Mgeni Rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd akipongezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF,Ndg. Aboubakar Rajab mara baada ya kutoa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) utakaoanza kufanyika kuanzia Februari 13,kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crenscentius Magori akitangaza majina ya washindi wa tuzo mbali mbali za NSSF kutoka mashirika,makampuni pamoja na watu binafsi.
Baadhi ya Washindi wa Tuzo mbali mbali za NSSF wakipokea tuzo zao hizo kutoka kwa Mgeni Rasmi katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd
Wakurugenzi Wakuu wa Zamani wakiwa na tuzo zao baada ya kupokea.
Mgeni Rasmi katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akiagana na Mke wa Makamu wa pili wa Zanzibar,Mama Asha Seif Idd.
Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka (kulia) akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira,Ndg. Eric Shitindi (katikati) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF,Ndg. Aboubakar Rajab.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF,William Erio (kulia) akimtambuliza Meneja Mawasiliano wa PPF,Lulu Mengele kwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe.
Zawadi kwa Mgeni Rasmi.
Zawadi kwa Mh. Waziri Kabaka.
King Kikii na Wazee Sugu.
Kigoma All Stars wakitigita stejini.
Mambo ya Kitamaa cheupee....


Wafanyakazi wa NSSF.
Wakurugenzi Wakuu wastaafu.
Wajumbe wa Bodi ya NSSF.

Waheshimiwa wabunge.
Wahariri wa vyombi vya habari hapa nchini.

Mambo yamenoga.
Picha ya pamoja na Baadhi ya Wakurugenzi wa Mifuko mbali mbali.
Picha ya pamoja na wakurugenzi wastaafu.
Picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya NSSF.
Picha ya pamoja na Wabumbe.

Picha ya pamoja na Washindi wa tuzo mbali mbali.