Monday, February 4, 2013

MAJAMBAZI WAVAMIA NYUMBANI KWA NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA NA MBUNGE WA BUMBULI(CCM), JANUARY MAKAMBA

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba
WATU wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamia nyumbani kwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba kwa lengo la kufanya uhalifu.
Hata hivyo majambazi hao ambao walimfunga kamba mlinzi wa nyumba hiyo na kuingia ndani, hawakufanikiwa kuiba chochote.
Naibu Waziri Makamba aliliambia gazeti hili kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana wakati yeye akiwa safarini jimboni kwake Bumbuli ila familia yake ilikuwapo nyumbani hapo.Makamba alisema baada ya majambazi hao kuingia ndani, walimfunga kamba na kumziba mdomo mlinzi.
“Ujambazi huo ulitaka kufanyika nyumbani kwangu Masaki karibu na Ubalozi wa Afrika Kusini. Mimi sikuwepo nyumbani. Walivamia chumbani mke wangu akabonyeza kengele iliyopiga kelele ndio wakakimbia, baada ya majirani kuwasili eneo la tukio, wakatokomea kusikojulikana,” alisema Makamba na kuongeza:
“Waliingia kwenye ofisi yangu ya pale nyumbani na kupekua. Lakini cha ajabu ni kwamba sebuleni kulikuwa na Ipad na laptop (kidadavuzi mpakato) lakini hawakuvichukua.”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyella alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watu hao walitaka kufanya ujambazi, lakini hawakufanikiwa.Kamanda Kenyella alisema tukio hilo lilitokea saa 10 alfajiri ya kuamkia jana, lakini majambazi hao hawakufanikiwa kutimiza azima yao.Kwa habari