Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa waganga wakuu wa mikoa , wilaya na baadhi wa wakurungezi wa hospitali za rufaa na taasisi za wizara hiyo wakiwemo wakurugnezi wa asasi za kiraia na wadau wa maendeleo.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akibadilishana mawazo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais , Mahusiano na Uratibu Uratibu ,Stephen Wasira katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wanawake, Sophia Simba akipongezwa na baadhi wabunge mara baada ya kuwasilisha hotuba yake ya Makadrio ya Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2013/2014.
Picha ya pamoja.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wanawake, Sophia Simba akifurahia jambo na Naibu wake mara baada ya kuwasilisha hotuba yake ya Makadrio ya Matumizi ya Fedha kwa wake 2013/2014. Picha zote na Magreth Kinabo – Maelezo
Naibu waziri wa Fedha Saada Mkuya
********************
Na Immaculate Makilika- Dodoma
SHERIA ya Madalali sura 227 (The Actioneers Act Cap.227) ni sheria iliyotungwa mwaka 1928 kama sura 282 ya Sheria za Tanganyika ,iliyofanyiwa marekebisho mwaka 1972 na mwaka 1994.
Sheria hii inatambua kuwepo kwa shughuli za dalali (Business of Auctioneer) kama mtu yeyote anayeuza (sells or Offers for Sale)mali yeyote inayohamishika au isiyohamishika (Movable or Immovable Property).
Sheria ya Madalali inampa mamlaka Katibu Mkuu Hazina ya kutoa leseni kwa madalali kupitia wilaya anayokaa mwombaji (resides) au anayotarajia kuweka shughuli zake za udalali.
Hayo yamesemwa Bungeni Dodoma na Naibu waziri wa Fedha Saada Mkuya ,alipokuwa akijibu swali la Mariam Kasembe (Masasi- CCM),swali lililohoji je, ni lini kutakuwaa na sheria ya kuwadhibiti madalali (Estate Agency ReguratoryBodies) kama ilivyo Kenya,Uganda na nchi nyingine za Afrika.
Aidha Mkuya aliendelea kwa kusema kwamba sheria yetu ya madalali haitoi mamlaka kwa madalali kufanya shughuli za upangishaji wa ardhi au majengo .”Sheria ya madalali haisimamii au kudhibiti mawakala wanaojishughulisha na uwakala wa majengo na ardhi (Estate Agents) alisema Naibu Waziri huyo.
Hata hivyo Mkuya aliendelea kwa kusema sheria yetu ya madalali ni ya muda mrefu ,miaka 85. Hivyo yako mambo mengi ambayo yamebadilika na kupitwa na wakati.
Kwa kutambua hilo,taratibu za kuifanyia marekebisho zimeanza .Baada ya kukamilika mawasiliano ndani ya Serikali muswada utaletwa Bungeni ili kukidhi mahitaji ya sasa na yajayo yanayohusiana na suala hili.
No comments:
Post a Comment