Na Mwandishi Wetu
KILE kinyang’anyiro cha kumsaka Redd’s Miss IFM kwa sasa kimefikia patamu, pale warembo 10 watakapoingia jukwaani Mei 25, mwaka huu kumsaka mrithi wa Fina Revocatus.
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika katika hoteli ya JB Bellmonte iliyopo Jengo la Golden Jubilee, maeneo ya Posta Mpya, Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es Salaam jana, Mratibu wa Redd’s Miss IFM, Daniel Sarungi alisema, mshindi wa taji hilo ataondoka na kitita cha Sh milioni 1.
“Warembo kumi ndio watakaoshiriki katika shindano hilo na mshindi ataondoka na Sh milioni 1, huku washindi wengine watatu tukitarajia kuwapa zawadi nyingine nzuri zaidi.
Meneja wa Redd’s Original walio wadhamini wakuu wa Redd’s Miss Tanzania, Victoria Kimaro alisema wanajivunia kuwa sehemu ya udhamini na wanaamini warembo hao watafanya kweli zaidi na kutwaa taji la Miss Tanzania.
“Hili shindano litakuwa moto, kwani tutalipa sapoti kubwa zaidi na kuhakikisha anatyoka mrembo atakayetwaa taji la Redd’s Miss Tanzania,” alisema Victoria.
No comments:
Post a Comment