Tuesday, July 2, 2013

WAMJUA COCO AUSTIN

Mwanamitindo Nicole Natalie Austin maarufu kama Coco Austin, amezaliwa mwaka 1979 huko Tarzana California.
Akiwa na miaka 18 alishinda Miss Ujena Mexico na ndio ukawa mwanzo wa kujulikana kwake,
amewahi kufanya kazi katika kampuni ya Playboy kwa muda wa miezi sita katika shughuli na sherehe zote 

za Playboy Mansion, amewahi kutokea katika filamu za Low-budget R-rated Films ikiwemo Southwest Babes (2001), Desert Rose (2002) na the Dirty Monks (2004)
Coco amewahi kutokea katika tv shows ikiwemo Hip-Hop Wives, the Comedy Central Roast of Flavor Flav, The Late Late Show with Craig Ferguson,The Dr. Oz Show, and Law & Order: Special Victims Unit.
Pia amewahi kutokea ukurasa wa mbele wa Playboy magazine ya March 2008 na michezo ya NBC Celebrity Family Feud June 24, 2008.
Coco ameolewa na rapa/ muigizaji Ice T mwaka 2001 uko Las Vegas na anatarajia kutimiza miaka 11 ya ndoa yake ifikapo tarehe 31 December mwaka huu.
Katika mahojiano na Mediaoutrage.com Coco alithibitisha kuwahi kufanyiwa upasuaji wa matiti na pia alikanusha kuwahi kufanya upasuaji wa kuongeza makalioo.
February mwaka huu ESPNRadio 1000 ya uko Chicago ilimtangaza Coco kuwa ndio mwanamke 'bomba' sana katika sayari hii.
Yeye na mumewe wanaishi uko Edgewater, New Jersey pia wana kipindi chao reality tv show kiitwacho ICE LOVES COCO..

No comments:

Post a Comment