Sunday, August 18, 2013

DAKTARI ANASEMA SINA UWEZO WA KUTIA MIMBA NA NYUMBANI NINA WATOTO WAWILI

Nikiwa njiani kutoka mahakamani kusikiliza hukumu ya rafiki yangu aliyehukumiwa miaka 30 nyuma ya nondo kwa - kesi ya kubambikiwa ya kum-baka msichana under 18, msichana mrembo ananiomba lifti, njiani anapoteza fahamu inabidi nimpeleke hospitali.

- Wakati akipata huduma ya kwanza hospitalini hapo, natumia simu yake kuwatafuta jamaa zake, nafanikiwa kuwapata wazazi wake.

-Wakati wazazi wake wanafika hospitali, daktari nae ndio anamaliza kumfanyia vipimo yule msichana na kutueleza kuwa ni mjamzito, muda mchache baadae msichana anapata fahamu, anaulizwa ujauzito wa nani? Msichana anaonyesha kidole kwangu.

-Lahaulaaa..najitetea.... Inabidi daktari anipime na mimi ili kuthibitisha madai ya msichana au la, baada ya dakika kadhaa daktari anakuja na majibu, vipimo vinaonyesha kwamba ile ya msichana hainihusu, vipimo vikasema zaidi, kwamba nina tatizo nililozaliwa nalo, kwamba sina uwezo wa kutia mimba.