Monday, August 26, 2013

WATOTO WA KIKE, TUWAFICHE WAPI WASIYAONE MAPENZI?


Mwanzoni mwa juma hili,nilitembelea shule moja ya wasichana nikiwa na shida ndogo ya kiofisi hapo.
Jina la shule naomba nilihifadhi sina taaluma ya uandishi wa habari,nisikiuke misingi yake.
...
Nilipofika ofisini nilikaribishwa staff ya walimu,nikaambiwa nisubiri.Hapo ndipo niliduwaa kumuona mwalimu mmoja wa kike akiingia ofisini na mtoto wa kike,kidato cha tatu huku akiandamwa na fimbo za mgongoni.
...
Tatizo lilikuwa kwamba,,yule binti alikuwa amekamatwa jumapili yake(siku iyo ilikuwa jumatatu)
Akiwa amelala na wanaume wawili wakati wenzake wameruhusiwa kwenda nyumba ya ibaada.Shule yenyewe ina taratibu ya kuwaruhusu wanafunzi kuhudhuria ibaada nje ya shule ambapo ni mwendo wa dk 25 ivi kwa miguu... Mwanafunzi huyu alikiri kulala na wanaume hao wawili na alipoulizwa aliwafaham vipi,alisema alitumia simu ambayo pamoja na shule kuzuia bado aliiweka kwenye taiti,,ikiwa na vibration.Aliweka wazi kuwa matroni hata akague vipi hawezi kuwakamata wote maana wanafunzi wengi wana simu.
...
Alipoulizwa anapaje ujasiri wa kulala na wanaume wawili,huku akilia anasema alikubaliana na mmoja,akaongezeka wa pili,,hivyo asingeweza kuwazuia.
...
Tukio hili ambalo bado linaendelea kuchukuliwa hatua stahiki ikiwemo wahusika kutafutwa,,lilinifanya niondoke na maswali mengi kichwani.Je tuwafiche wapi? Je malezi gani tuyatumie? Je wazazi walio nyumbani wanajua watoto wao wanamiliki simu? Je imefika mahali,somo la Mahusiano Urafiki Mawasiliano na Mapenzi liwekwe shuleni? Je hawa ndo wake wema na waume wema wa kesho?
Iliniuma,,jamani tusitafute wa kulaumu bali nini kinaweza kuleta usalama.