Wednesday, September 4, 2013

SIRI YAFICHUKA: KISA CHA AUNT EZEKIEL KUPIGWA CHUPA NI PENZI LA JEFF LINALOGOMBANIWA NA WAREMBO

Siri ya Aunt Ezekiel kupigwa chupa club na kujeruhiwa mkono wake imefichuka.Habari za uhakika zinadai kwamba Aunt alipigwa chumba na mrembo wa kike katika harakati za kugombea penzi la mwanaume...

Mwanaume aliyekuwa akigombaniwa ni Jeff ambaye anadaiwa kuwa ni boyfriend wa Yvonne ( aliyempiga aunt chupa )..

Kutokana na aibu hiyo, mastaa kadhaa wameongea na mpekuzi kwa nyakati tofauti na kueleza masikitiko yao dhidi ya aunt Ezekiel ambaye ni mke wa mtu... 

Katika maongezi hayo, mastaa hao walidai kwamba mambo anayofanya aunt hayaendani na matendo ya mke wa mtu. Aunt amekuwa ni mtu wa baa, club na madanguro mengine ya usiku, hali inayotia shaka uhai wa ndoa yake. 

" Aunt kapata mume mwelewa sana ambaye kakiheshimu sana kipaji chake kwa kuto-mbana.

"Cha ajabu yeye ameanza kufanya mambo ya aibu kwa kuendekeza ngono nje ya ndoa yake" alisema star mmoja wa kike aliyekataa kuwekwa wazi jina lake ..

Muigizaji mwingine wa kike ambaye hakuwa tayari kuchorwa mtandaoni alisema:

"Aunt ajiangalie sana.Yeye ni mke wa mtu kwa sasa. Kitendo alichokifanya kimemchafua mpaka ukweni na asipokuwa makini atampoteza mume wake...

"Yvonne alikuwa anamlinda bwanake, mi siwezi kumlaumu sana ila nyie wanaume ni watu wabaya sana pia"

No comments:

Post a Comment