Tuesday, October 29, 2013

BATULI AFUNGUKA KUHUSU MADAI KUWA IRENE UWOYA ANAMUENDEA KWA WAGANGA ILI AMPOTEZE KWENYE FILAMU

Siku za Hivi karibuni kumekuwa na tetesi zisizo rasmi kuwa mastaa wawili wa filamu Swahiliwood Yobnesh Yusuph(Batuli) na Irene Uwoya hawana maelewano mazuri chanzo kikidaiwa ni Irene Uwoya kutaka kumpoteza Batuli kwenye tasnia ya filamu ili asifurukute. Habari hizo zinaenda mbali zaidi zikidai kuwa kuna kipindi Batuli alikuwa anaumwa maeneo ya kifuani lakini baadhi ya watu wakiwemo wasanii wenzake wakiamini Uwoya ndiye kamfanyia mambo ya kilozi(ushirikina). 

Tetesi hizo tulizipuuza mwanzoni lakini zinaonekana kurudi tena kwa kasi hivyo tuliamua kuwatafuta mastaa hao wawili ili watoe ufafanuzi wao wenyewe na wa kwanza kuulizwa alikuwa Uwoya hata hivyo namba yake ilionekana kutokuwa hewani alipotafutwa juzi na jana alipotumiwa ujumbe namba yake ilionekana bado haipo hewani. Batuli nae alitumiwa ujumbe juzi kuhusu issue hiyo lakini hakujibu mpaka jana usiku ndiyo alijibu akisema alikuwa busy sana. Batuli alisema "sina ubaya na msanii yeyote na moyo wangu ni mweupe na nina mapenzi na wasanii wenzangu wote, nawapenda sana anayeniwinda kwa ubaya Mungu atanipa ulinzi wake, sipendi uadui na mtu namuachia Mungu atanilipia yote"