Thursday, October 17, 2013

KAMA ULIMISS SHOW YA WEMA SEPETU"IN MY SHOES" KWENYE TV JANA, HAYA NDIYO YALIYOJIRI .

Show ya TV ‘In my shoes’ ya mwigizaji Wema Sepetu kutoka bongo movie imeanza kuonyeshwa Eatv October 16 2013 ambapo Episode hii ya kwanza imeanza kwa kumuonyesha Wema kwanza akieleza yeye ni nani, anafanya nini, ni mtu wa aina gani na mengine kama hayo ambapo yafuatayo hapa chini ni maswali aliyoulizwa na kuyatolea majibu.


Swali: Wema ni nani?


Jibu: Wema Sepetu is a girl, i can say a Lady mwenye umri wa miaka 24 kutoka familia ya Isack Abraham Sepetu, a darling, a libra.. a girl who is very ambicious, i love my self…


Swali: Siku yako ya kwanza shuleni ilikuaje?


Wema: Siku ya kwanza tumeenda nikakutana na msichana flani hivi anaitwa Shubira nakumbuka mpaka leo, alikua rafiki yangu wa kwanza tulikutana shuleni nilikua na miaka minne… tumekaa nikaanza kulia kwa sababu ilikua sehemu mpya, mazingira mapya baada ya hapo tukazoea.


Shule ilikua vipi kipindi unasoma?


Wema: Naweza kusema kipindi ambacho niko shule, Mwalimu wangu sijawahi kukaa hata siku moja kumfikiria mara mbili na haijawahi kutokea kwamba hata mwalimu akaweza kufanya labda matamanio au kutaka kitu chochote, hamna kitu kama hicho


Swali: Utafanya nini ikitokea umerudi shule?


Wema: Ningepata nafasi ya kurudi shule, academic nini uniform na nini… ningejaribu kuifanya more fun, a place where everybody can be just himself or herself and just be Wema Sepetu kwa sababu right now this is my time!!


Swali: Ni nani ambae uko karibu nae kwenye familia yenu?


Wema: Dada yangu wa kwanza kuzaliwa anaitwa Tunu, tunakwenda sawa kwenye many many ways, kipindi mama yangu alivyonizaa aliumwa akalazwa hivyo dada yangu ndio akawa ananihudumia kama mtoto wake, ananinywesha uji… anahakikisha nimekunywa maziwa on time na mpaka leo ananiita my baby and I call her my mami… mtu wa pili ni dada yangu wa tatu, she is my bestfriend… baba yangu atabaki kuwa baba yangu tu, mama yangu ni my gurdian Angel, my heart my darling.

Swali: Ulishawahi kugombana na ndugu zako?


Wema: Yeah nimegombana na dada yangu mpaka sasa hivi hatuongei, sio kitu chepesi….


Swali: Unaamini Mama yako ni mkorofi?


Wema: Linapokuja swala la mama yangu huwezi ukasema kwamba ni mkorofi lakini hapendi nikikosea wala kufanya kitu ambacho sicho…. kutokupenda kwake inafikia point anakua na hasira sana alafu njia ya kuonyesha hasira yake ndio level ya juu, yeye anafikiria kwamba anatengeneza ila badala ya kutengeneza ndio anaharibu.


Swali: Wema ni mkorofi?


Wema: Mimi sio mkorofi, mtu ambae hanijui ndio ataniita mkorofi ukishanijua yani tutafika mbali lakini usiponijua na hujui ninachonitaka ndio tatizo.


Swali: Unajisikiaje kuwa Wema Sepetu?


Wema: Kuwa Wema Sepetu sio kitu rahisi, haiwezi kuwa kama watu wanavyofikiria na haitakua hivyo kwa sababu ni maisha ambayo naishi, ni mpaka uone maisha ninayoishi ndio unielewe… yani hata kujaribu kuieleza ili uielewe napata tabu… mashabiki wangu wananielewa sana na uhusiano wangu na wao ni mzuri na ni tofauti na uhusiano kati yangu na familia yangu’Swali: Unachukulia vipi unaposemwa ama kuandikwa vibaya?


Wema: Katika vitu vyangu ambavyo mtu wa nje anaweza kuviona kama vile… Mungu wangu Wema ana nini, mi navichukulia kama changamoto… mi naona kuna kitu special kuhusu mimi, kwa nini wasiseme watu wengine?


Swali: Unaamini wewe ni mrembo?


Wema: I am beautiful, naamini kwamba mimi ni beautiful kwa sababu nina pure heart… ni kitu Mwenyezi Mungu alichonibariki nacho.