Wednesday, October 2, 2013

MWANAFUNZI WA MIAKA 13 AJIFUNGUA MTOTO WA MIEZI 6 SEBULENI BILA KUJIJUA


MWANAFUNZI WA MIAKA 13 AJIFUNGUA MTOTO WA MIEZI 6 SEBULENI BILA KUJIJUA
MSICHANA aliyejitambulisha kwa jina la Salma Hemedi (13) mwanafunzi wa Shule ya Msingi Ubungo Plaza, Dar amejifungua maiti ya kichanga cha miezi 6 bila mwenyewe kujijua.
Tukio hilo lilitokea Septemba 25, mwaka huu maeneo ya Ubungo National Housing jijini Dar ambapo asubuhi ya siku hiyo, Salma alilalamikia maumivu ya tumbo lake kiasi cha mama yake aliyejitambulisha kwa jina la Rahma Shabani kwenda kuomba msaada wa kitabibu.
Mwanamke huyo alieleza kwamba baada ya kurudi ndani alikomuacha mwanaye, alimkuta akiwa amejifungua kichanga sebuleni, kitu ambacho hakukitarajia kwa kuwa alizoea kumnunulia vifaa vya kujisitiri wakati wa hedhi kila alipomlalamikia maumivu ya tumbo akijua yupo kwenye siku zake.
Akiwa na manesi walioongozana naye, walimsaidia Salma huku kila mtu akiwa amepigwa na butwaa kwa kilichotokea kwani hakuna aliyekuwa anajua kama Salma alikuwa na ujauzito.
Akiongea na waandishi wetu, Salma alisema alipewa ujauzito na mwanaume aliyemtaja kwa jina la John Vicent ambaye alikuwa mtoto wa mwenye nyumba wao wa zamani.
Salma alisema kuwa John alikuwa akimshawishi kila mara kufanya mapenzi japo alimkatalia kwa kuwa alijua akifanya kitendo hicho atapata mimba. 
Salma alizidi kutiririka kuwa John alikuwa akimpa dawa alizodai ni za kuzuia ujauzito. 
Baada ya kupata taarifa hizo mama wa Salma pamoja na ndugu zake walitoa taarifa Kituo cha Polisi Urafiki ambapo walifungua jalada la mashtaka lenye namba RB, URP/RB/7316/2013 KUBAKA na kupewa PF3 kwa ajili ya matibabu na uthibitisho wa daktari.
Walimu wa shule anayosoma Salma, walipigwa na butwaa baada ya kupata taarifa hizo na kueleza kwamba hawakuwa na taarifa kwamba denti huyo alikuwa mjamzito.
Kichanga hicho kilizikwa makaburi ya Ufi, Shekilango jijini Dar.