Tuesday, October 8, 2013

WATOTO WASEMA HAYA TUMECHOKA

HALI inatisha! Kundi la vijana wahuni lililopo maeneo ya Mgeninani, Mbagala-Kuu jijini Dar, linadaiwa kuhusika katika vitendo vya kulawiti wanafunzi wa shule za msingi na chekechea zilizopo maeneo hayo na kusababisha madenti hao kusema: “Tumechoka kulawitiwa!”
Awali ‘makamanda’ wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) walipokea taarifa kutoka kwa mmoja wa wazazi waliolalamikia watoto wao kulawitiwa na vijana hao na kuwaomba wafike eneo hilo ili kukomesha matukio hayo.
Baada ya kupata taarifa hizo, timu ya OFM ilitinga maeneo hayo na kuthibitisha kuwepo kwa matendo hayo ambapo iliwasaidia wazazi hao kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Mbagala-Kizuiani kisha wakapatiwa PF-3 kwa ajili ya matibabu na uchunguzi wa kitabibu na kuandaa utaratibu wa kuwakamata watuhumiwa.
Wakizungumza na OFM, wanafunzi hao waliodaiwa kulawitiwa waliwataja watuhumiwa wawili kwa jina mojamoja ambao ni Side na Mudi.
Walidai kuwa vijana hao huwachukua wakati wa kutoka shuleni na kuwapeleka kwenye majumba mabovu kisha kuwaingilia kwa zamu huku wakiwachezea sehemu za siri na kuwapa shilingi mia mbili wakiwaonya kutunza siri. 
Wanafunzi hao ambao wengi wana umri chini ya miaka 15 wa shule ya msingi na chekechea, waliendelea kutiririka kuwa wamekuwa wakilawitiwa na wanaume hao kwa takriban miaka miwili na kukiri kuficha siri hiyo kwa kuogopa kudhuriwa na wahusika.
Miongoni mwa wanafunzi waliofanyiwa unyama huo ni denti wa darasa la nne (14), mwingine wa chekechea (7), wa darasa la pili (8) na mtoto mdogo wa kiume (4) ambao wote majina yanahifadhiwa kwa sababu za kimaadili.
Kwa mujibu wa Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Maendeleo, Mteghenjwa Kidika ambaye baadhi ya wanafunzi waliofanyiwa unyama huo ni wa shule anayosimamia, alikiri kuwepo kwa hali hiyo tete.
Alisema wanafunzi hao walio chini ya darasa la tano hufanyiwa vitendo hivyo kwa kuwa hawapatiwi nasaha tofauti na wale wa darasa la tano hadi la saba wanaopewa elimu hiyo.
Baada ya kufanyiwa uchunguzi kwa vipimo vya daktari katika Hospitali ya Mbagala-Zakhem, Dar ilibainika kuwa walikuwa wamepata madhara makubwa sehemu za siri.

OFM iliweka kambi kwa muda wa siku mbili ikiwa na wazazi na jeshi la polisi ambapo ilifanikiwa kumnasa mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Said na kufikishwa katika Kituo cha Polisi Kizuiani-Maturubai na kufunguliwa jalada la kesi namba MB/RB/10209/2013 ULAWITI huku wengine wakiendelea kusakwa.