Wednesday, November 20, 2013

KAJALA KESI UPYAAA...HUKUMU IKO TAYARI...WEMA ASHANGAA!!!! SOMA ZAIDI

AMA kweli hujafa hujaumbika! Bado bundi anamnyemelea staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja baada ya kurejeshwa kortini kwa mara nyingine huku kesi ikimjia upya, Risasi Mchanganyiko limesheheni.

Kajala Masanja.MUME AKATA RUFAA
Pamoja na kutoa faini ya Sh. milioni 13 alizolipiwa na staa mwenzake wa filamu, Wema Isaac Sepetu, Kajala anatarajiwa kuhukumiwa tena Novemba 25, mwaka huu baada ya mumewe, Faraji Agustino Chambo kukata rufaa katika mahakama kuu.

Kwa mujibu wa jaji aliyezungumza na gazeti hili, kuna kila dalili wawili hao wakaachiwa huru au wakafungwa tena kwa adhabu kubwa zaidi ya ile ya awali, hivyo huu ni msala mpya kwa Kajala ambaye tayari alikuwa uraiani.
Kesi iliyokuwa ikiwakabili wanandoa hao ilihusiana na utakatishaji wa fedha haramu uliofanywa na mume wa Kajala wakati akifanya kazi kwenye Benki ya NBC, Dar.

Mume wa staa huyo ndiye anadaiwa kukata rufaa wakati akitumikia kifungo cha miaka saba jela baada ya kukutwa na hatia.

Habari za ndani zilieleza kwamba, Kajala alisharidhika na hukumu iliyotolewa Machi 25, mwaka huu ambapo yeye alitakiwa kufungwa mitatu au kulipa faini ya shilingi milioni 13.

Katika hukumu hiyo, mume wa Kajala alifungwa miaka saba na ndipo alipoamua kukata rufaa na akamuingiza Kajala kwa maelezo kuwa wote hawakuridhishwa na hukumu iliyotolewa mwanzoni.

Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Kajala, staa huyo amekuwa katika wakati mgumu na mara nyingine na kujikuta akiangua kilio hasa anapokumbuka maisha ya gerezani.

KAJALA KORTINI

Ili kuthibitisha habari hizo, juzi (Jumatatu) Kajala akiwa na shosti wake, Wema anayehaha kumnasua, alipigwa chabo na mashushushu wetu wakitinga tena katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Habari zilieleza kuwa jaji ambaye alikuwa akipitia ya hukumu ya awali ya wanandoa hao, alidai kwamba Jaji Temba aliyetakiwa kutoa hukumu ya kesi hiyo upya alikuwa anaumwa.

HUKUMU NOVEMBA 25

Kufuatia kuumwa kwa hakimu huyo, kesi hiyo iliahirishwa hadi Novemba 25, mwaka huu, ambayo itakuwa siku ya hukumu huku ikielezwa kuwa kila kitu kipo tayari.

Akiwa katika viunga vya mahakama hiyo, Kajala alionekana mwenye wasiwasi na woga kwa sababu hakuwa anajua kama anaweza kuburuzwa kortini kwa mara nyingine kuhusiana na suala hilo kwa kuwa aliamini alishamaliza kwa kulipa faini ya Sh. milioni 13 kisha kurejea uraiani huku mumewe akienda jela.

Kajala alisema anaomba Mungu ili kikombe hicho kimuepuke kwani alishasahau kama anaweza kurudi kortini.

“Sikudhani kwa kweli kama ninaweza kurudi mahakamani, Mungu anisaidie kwa kweli…” alisema Kajala.

Naye Wema alipigwa na mshangao baada ya kuona kesi hiyo imeibuka tena.

“Siku ile niliuliza kilikuwa kinahitajika nini ili Kajala awe huru, nikaambiwa milioni 13, nikatoa, sasa iweje tena arudishwe mahakamani?” alihoji na kuonesha wasiwasi mkubwa baada ya kuambiwa kuwa Kajala anaweza kufungwa kwa kuwa hukumu inapitiwa upya.

Wakili wa Kajala, Peter Kibatala alisema anapambana kunyoosha sheria kuhakikisha mteja wake anakuwa huru.

No comments:

Post a Comment